Jaji Mkuu awaonya viongozi wa serikali na wanasiasa

In Kitaifa
Jaji Mkuu wa Tananzania, Profesa Ibrahimu Juma amewataka viongozi wa serikali na vyama vya siasa kuacha mara moja vitendo vya kuingilia mhimili wa Mahakama na kuvunja amri zake.
Jaji Profesa Juma ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu wiki ya Sheria inayotarajiwa kufanyika mwanzoni mwa mwezi ujao (Februari mosi), siku ambayo ndio itakayoashiria kuanza rasmi kwa shughuli za Mahakama kwa mwaka huu 2018 yatakayofanyika katika viwanja vya Mahakama vilivyopo mtaa wa Chimala jijini Dar es Salaam, ambapo mgeni rasmi atakuwa Rais John Magufuli.
“Kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania mamlaka ya utoaji haki ni ya Mahakama tu, nawasihi viongozi wote wa serikali wenye mamlaka za kikatiba na kisheria wabaki ndani ya maeneo yao ya Kikatiba na wajiepushe kuingilia maeneo yaliyo ndani ya haki, hadhi na Mamlaka ya Kikatiba ya Mahakama”, alisema Jaji Profesa Juma.
Kwa upande mwingine, Jaji Profesa Juma ametoa rai kwa wananchi na wadau wote wa sheria kutembelea Mnazi Mmoja kwa ajili ya kujifunza na kupata huduma mbalimbali za Kisheria kutoka kwa Majaji, Mahakimu, Wasajili, Watendaji, Mawakili wa serikali na Mawakili wanaojitegemea ambao watakuwa tayari kuwasikiliza na kuwahudumia ipasavyo.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu