Jaji Mutungi avitahadharisha vyama vya siasa.

In Kitaifa

Vyama vya siasa nchini vimetakiwa kutekeleza majukumu yao ya kisiasa kwa kufuata na kuzingatia sheria na kanuni za vyama vya siasa na si vinginevyo.

Agizo hilo limetolewa na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Tanzania, Jaji Francis Mutungi kufuatia tabia iliyojitokeza  ya baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa nchini kutumia vibaya vyombo vya habari, hususani mitandao ya kijamii kufanya vitendo au kutoa kauli ambazo zinavunja sheria za nchi.

“Ninasisitiza kuwa viongozi wa vyama vya siasa wasitumie vibaya dhana ya demokrasia na uhuru wa habari, kuvunja Sheria za nchi. Ieleweke kwamba mtu yeyote anapokiuka sheria za nchi, Sheria itachukua mkondo wake bila kujali wadhifa wa mhusika katika chama cha siasa, amesema Jaji Mutungi.

Hata hivyo, Jaji Mutungi ametoa rai kwa viongozi wote wa vyama vya siasa na wanachama wote wa vyama vya siasa nchini kuheshimu sheria za nchi wakati wote ili kudumisha na kukuza demokrasia ya vyama vingi nchini.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Hamas yatangaza kusitisha mapigano.

Chama cha Wapalestina cha Hamas kinachotawala Ukanda wa Gaza kimetangaza uamuzi wa upande mmoja wa kusitisha mapigano, baada ya

Read More...

Upinzani Congo wagawanyika

Wafuasi wa chama cha UDPS nchini Kongo wamesifu hatua ya kiongozi wao Felix Tshisekedi kujiondoa kwenye mkataba wa viongozi

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu