Jeshi la Mali lauwa wapiganaji 30

In Kimataifa

Vikosi vya mali vimewauwa kiasi ya wanamgambo 30 katika operesheni yake iliyoendeshwa jana, hayo yakiwa ni machafuko ya hivi karibuni kabisa katika taifa hilo lililovurugwa na vita. Katika ukurasa wake wa Twitter jeshi la nchi hiyo limesema limefanya mauwaji hayo katika eneo na Burkina Faso. Na kuongeza kwamba limefanikiwa kuzikamata pikipiki 25 na vifaa vingine, pasipo kutoa taarifa zaidi. Mali imekuwa katika makabiliano na wimbi la wapiganaji wenye itikadi kali za Kiislamu lililozuka 2012, ambalo limegharimu maelfu ya maisha ya wanajeshi na raia tangu wakati huo. Pamoja na uwepo wa maelfu ya wanajeshi wa Ufaransa na vikosi vya Umoja wa Mataifa machafuko yameendelea na yameenea katika mataifa jirani ya Burkina Fasi na Niger.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Mgombea urais wa chama tawala Burundi atangazwa mshindi kwa kupata asilimia 68.7

Mgombea urais wa chama tawala nchini Burundi Evariste Ndayishimiye ametangazwa mshindi leo kwenye kinyang’anyiro hicho ambacho kimedaiwa kukumbwa

Read More...

Watu 7 Wanaodhaniwa Kuwa Majambazi Wauawa Dar es Salaam

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kuwaua majambazi saba na kufanikiwa kukamata silaha ndogo Bastola

Read More...

Watanzania watakiwa kucheki afya zao na kufuata ushauri wa daktari.

Watanzania wametakiwa kuwa na mazoea ya kwenda vituo vya afya kucheki afya zao na kuacha dhana ya kutumia

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu