Jeshi la Sudan lakemewa kushambulia waandamanaji.

In Kimataifa

Jeshi la nchini Sudani limekemewa kutokana na mashambulizi yake dhidi ya waandamanaji mjini Khartoum, hatua iliyosababisha watu 30 kupoteza maisha.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametaka uchunguzi ufanyike akisema ametamaushwa na ripoti kuwa maafisa walifyatua risasi hospitalini.

Marekani na Uingereza zimesema ni ”tukio la kikatili”.

Sudan imekua chini ya utawala wa kijeshi tangu Rais Omar al-Bashir alipopinduliwa mwezi Aprili.

Viongozi walioongoza vuguvugu la kutaka utawala wa kiraia kuongoza nchi hiyo, wamesema wamesitisha mawasiliano na serikali ya mpito ya kijeshi na kufanya mgomo.

Vikosi vya usalama vilifika maeneo ambayo watu walikua wakiandamana, mapema Jumatatu na sauti za risasi zilisikika kwenye picha za video.

Katika taarifa yake iliyosomwa kwa njia ya televisheni ya taifa, Jeshi limeeleza masikitiko yake kwa namna hali inavyozidi kuwa mbaya na kusema kuwa operesheni ilikua imewalenga ”wanaotia dosari hali ya usalama na wahalifu’

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

MBUNGE JAGUAR WA KENYA ALIYETISHIA KUWAFURUSHA WATANZANIA AKAMATWA

Maafisa wa polisi nchini Kenya wamemkamata mbunge wa jimbo la Starehe anayedaiwa kutoa kauli za chuki dhidi ya wafanyabiashara

Read More...

MANCHESTER CITY, YAMTOA KAFARA DANILO

. . Klabu ya Manchester City, ipo tayari kutoa kiasi cha paundi milioni 44 na beki wao wa pembeni

Read More...

TOTTENHAM MBIONI KUMSAJILI KIUNGO KUTOKA LYON.

. . Klabu ya Tottenham, imekubali kutoa kitita cha kiasi cha paundi milioni 62 kumsajili kiungo wa kati wa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu