Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Nchini, liko katika mkakati wa kuingia ushirikiano na Serikali ya Kuwait

In Kitaifa

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Nchini, liko katika mkakati wa kuingia ushirikiano na Serikali ya Kuwait, katika shughuli zake za kukabiliana na majanga ya moto ikiwa ni juhudi zake katika kuyafikia maeneo mengi nchini.

Hayo yamejiri baada ya Balozi wa Kuwait Nchini, Jasem Al-Najem alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji jijini Dar es salaam, ambapo ameeleza kuwa serikali ya Kuwait ipo tayari kubadilishana mafunzo na kutoa msaada wa vifaa kwa Jeshi hilo.

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye amemshukuru kwa kumtembelea na kusema kuwa ujio wa balozi huyo, umefungua ukurasa mpya kwa upande wa misaada na mafunzo kwa Askari wa Jeshi hilo, kwani watapata fursa ya kubadilishana uzoefu na kuongeza tija kwa Jeshi lake.

Katika kikao hicho Balozi wa Kuwait, Nasem Al-Najem alipokea taarifa ya changamoto zinazolikabili jeshi hilo ikiwemo uhaba wa vitendea kazi ,huku akiahidi kuzifanyia kazi na akisisitiza mchakato wa kusaini makubaliano ya hiari ukamilike kwani utakuwa msaada wa kutekeleza kwa haraka program za mafunzo ya muda mfupi.

 

 

 

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu