Jokate Mwegelo OUT.

In Kitaifa, Siasa
Kamati ya Utekelezaji ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi(UVCCM), imetengua uteuzi wa nafasi ya Kaimu Katibu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi wa Umoja huo iliyokuwa ikiongozwa na  Jokate Mwegelo .
Jokate aliteuliwa Aprili mwaka jana na Kamati hiyo kukaimu kwa muda kabla ya kamati hiyo kufanya uchaguzi.
Kaimu Katibu Mkuu Taifa wa Umoja Shaka Hamdu amekiri Jokate  kutenguliwa kwa nafasi hiyo leo Machi 25,  2018 kupitia vikao vya Kamati vilivyokutana kwa mujibu wa kanuni na taratibu za UVCCM.
“Kwanza ifahamike Jokate aliteuliwa kukaimu kwa utaratibu wa UVCCM  na ameondolewa kwa utaratibu, ni kama alikuwa kwenye majaribio,” amesema Shaka.
Shaka amesema utaratibu wa kujaza nafasi hiyo utafanyika hapo baadaye kupitia vikao vya umoja huo.
Uteuzi wa Jokate kuwa Kaimu Katibu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipkizi, ulionekana kutaka kuivuruga jumuiya hiyo baada ya kuibuka mjadala kwa viongozi na wanachama wakidai uteuzi huo haukufuata kanuni na taratibu za umoja huo.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu