JPM:Wasemaji wenu wawe viongozi wa Dini.

In Kitaifa

Rais John Magufuli amewataka viongozi wa dini kuwa wasemaji wa mambo yao na si kusemewa na wanasiasa.

Amesema hayo leo Juni 12, 2018 alipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa msikiti mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), unaojengwa Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Rais amesema viongozi wa dini wanapaswa kuwa wasemaji wakuu wa mambo yao na si kuwaachia watu wengine ambao hawana uhusiano wowote na masuala ya kidini.
“Msiwe na wasemaji ambao si viongozi wa dini. Msiwatumie wanasiasa… mambo ya dini yazungumzwe na viongozi wa dini wenyewe,” amesema Rais Magufuli.
Amesema kuwapa uwanja wanasiasa kuwa wazungumzaji wa masuala ya kidini kunaweza kulitumbukiza Taifa katika hatari kwa kuwa wanasiasa wamekuwa na tabia ya kutaka kutumbukiza ajenda zao.
“Msitafute wasemaji kwa niaba ya maaskofu, mapadri, wachungaji, masheikh… kuweni wasemaji wa mambo yenu wenyewe. Mtakuwa mnatupoteza, Taifa mtalipeleka kubaya. Mambo yenu yasemeeni wenyewe kuwapa watu wengine mtawachanganya wasikilizaji,” amesema.
Rais Magufuli amemkabidhi Sh10 milioni kwa Mufti wa Tanzania, Abubakary Zubeiry zikiwa mchango wake katika kugharimia ununuzi wa saruji ili kuharikisha ujenzi wa msikiti huo unaotarajiwa kumalizika Aprili, 2019.
“Hela hii ikasaidie kununua mifuko 625 ya saruji ili msikiti huu ukamilike kwa wakati… nafahamu ujenzi wake unagharimiwa na Mfalme wa Morocco lakini nami nimeona nichangie sehemu hiyo ndogo,” amesema.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Mwanamfalme Saudia Kuchunguzwa kifo cha Khashoggi.

Kuna ushahidi kamili kwamba mwanamfalme wa Saudia Mohammed bin Salman na maafisa wengine wa ngazi za juu wanahusika kibinafsi

Read More...

Hafla ya kutambulisha tuzo ya serengeti yafanyika.

Waziri wa maliasilai na utalii Mh Hamis Kigwangala leo ameshiriki katika zoezi la utambulishwaji wa Tuzo ya Mbuga ya

Read More...

Serikali inadaiwa zaidi ya bilioni 6.

Shirika la Uzalishaji Mali la Magereza kupitia Jeshi hilo limeiomba Serikali kuwalipa deni la shilingi Bilioni 6.45 fedha zilizotumika

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu