Julio amewataka viongozi wa klabu za soka nchini kuacha kasumba

In Michezo

Aliyewahi kuwa kocha wa vikosi vya Simba Sc, Mwadui Fc na
Dododma Fc Jamuhuri Kiwelu Julio amewataka viongozi wa
klabu za soka nchini kuacha kasumba ya kujibebesha jukumu la
kufanya usajili, ili kutoa nafasi kwa benchi la ufundi kutimiza
wajibu wake kitaaluma.


Soka la Tanzania kwa muda wa miaka nenda rudi limekua na
malalamiko kuhusu mfumo wa usajili ambao haufuati taaluma
na ushauri kutoka kwenye benchi la ufundi, na kusababisha
makocha kufanya kazi zao ipasavyo na mwishowe kufukuzwa.
Kocha Jamuhuria mbaye kwa sasa hana timu ya kufundisha,
amesema kutokana na hali hiyo viongozi wamekua chanzo cha
kuharibu muendelezo ya timu za tanzaniakufanya vizuri, kwa
kufanya usajili wa kishabiki na kutanguliza ubinafsi.

Julio amesema kazi kubwa ambayo inapaswa kubaki kwa
viongozi endapo watakubali kuachana na kasumba ya kuingilia
majukumu ya benchi la ufundi, ni kufanikisha makubaliano kati
ya klabu na mchezaji aliyependekezwa na kocha kupitia ripoti
yake, baada msimu ama wakati wa dirisha dogo la usajili.


Julio ametoa ushauri huo, huku akipongeza mfumo ulioanza
kufanyiwa kazi na uongozi wa klabu ya Simba kupitia idara ya
mtendaji mkuu ambayo aawali ilikua ikiongozwa na Crecentiua
Magori na baadae kukabidhi kijiti kwa Senzo Mazingiza.


Hata hivyo Julio amethibitisha kuwahi kukutana na changamoto
kadhaa kutoka kwa viongozi wa klabu ya Simba wakati akiwa
kocha wa kikosi cha  klabu hiyo, lakini anaamini msimamo wa
kutaka taaluma yake iheshimiwe ndio iliyosababishwa
akaondolewa klabuni hapo na mpaka leo hatakiwi.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu