Kagere amjibu Makambo

In Michezo

MSHAMBULIAJI wa Simba, Mnyarwanda, Meddie Kagere amemchimba mkwara mpinzani wake katika mbio za kuwania ufungaji bora wa Ligi Kuu Bara, Harietier Makakambo wa Yanga kwa kusema kuwa hata afunge mabao mangapi lakini hawezi kutwaa tuzo hiyo zaidi yake.

Kagere mwenye mabao 14 akizidiwa bao moja na Makambo mwenye mabao 15 wakati anayeongoza ni mshambuliaji wa Mwadui, Salim Aiyee akiwa amefunga mabao 16 licha ya timu yake kuwa katika nafasi ya 14 katika msimamo wa Ligi Kuu Bara kutokana na kuwa na pointi 37.

Kagere alisema kuwa hawezi kuwa na presha na suala la ufungaji katika ligi kuu kutoka kwa wapinzani wake akiwemo Makambo kutokana na kuamini nafasi kubwa ipo kwake.

“Siwezi kuwa na presha ya nani amefunga mabao mangapi kwa sababu hii ni ligi na kila mmoja anacheza kwa kuipambania timu yake hivyo kwangu naona ni jimbo la kawaida kwa kuwa bado nina nafasi kubwa ya kuweza kufunga mabao zaidi ya wao kulingana na mechi zilizopo mbele yetu.

“Najua nini cha kufanya ili kuweza kutimiza hilo, mabao nitafunga na nitakua juu ya hao ambao wamenizidi, yeye namuacha aendelee kufunga na nitafunga yangu kutokana na ushirikiano ninaoupata kutoka kwa wachezaji wenzangu hilo halitokuwa na shida ni suala muda kufika tu,” alisema

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Baraka da Prince sasa kufunga ndoa na Naj

Msanii wa Bongo fleva Baraka de Prince amebainsha wazi kufunga ndoa mwaka huu na mpenzi wake Naj. Minong’ono ilikua

Read More...

Ajibuawataka Simba watulize boli, msimu ni wao

Nyota wa Simba, Ibrahim Ajibu amesema kuwa mashabiki wa Simba watulie watakubali mziki wake kwani amejipanga kufanya maajabu. Ajibu

Read More...

Waziri Mkuu kuzindua Daftari la kudumu la kupiga kura.

Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC Dkt Athumani Kihamia, amesema zoezi la uandikishaji wa daftari la Kupiga

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu