Kamanda Shanna afanya msako mkali, akamata Ak47 na meno ya tembo

In Kitaifa

Jeshi la polisi Mkoani Arusha limeendelea kuwasaka walifu wa matukio mbalimbali ili kuweza kuleta amani wa wananchi wake

Akizungumza na vyombo vya habari kamanda wa jeshi la polisi mkoani Arusha Jonathan Shanna amethibitisha kukamatwa kwa mtu ajulikanae kama Solomon Letato akiwa na silaha aina ya Ak47 pamoja na risasi 5 zilizokuwa kwenye magazine

Kamanda amesema kuwa mtuhumiwa huyo ana umri wa miaka 30 ambae ni mwalimu wa shule ya msingi NAAM iliyopo kata ya Enguserosambu tarafa ya loliondo wilaya ya Ngorongoro ambapo silaha hizo alikuwa anafanyanazo biashara haramu ya kuuwa tembo na pembe za faru na shughuli nyingine za ujangili

Aidha katika tukio lingine jeshi la polisi limefanikiwa kukamata silaha silaha nyingine aina ya ak47 ambayo ametelekezwa katika kijiji cha Mbukeni kata ya Arashi tarafa ya Loliondo ikiwa na risasi moja

Katika tukio lingene jeshi la polisi limefanikiwa kuwamata majangili sugu na hatari 3 wa akiwa na nyaraka za serikali katika kitongoji cha Maji ya chai kata ya maji ya chai tarafa ya kingori wilaya ya Arumeru wakiwa na vipande 4 vya meno ya tembo walivyokuwa wamehifadhi kwenye mfuko wa sandarusi

Kamanda Jonadhan amesema wamefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 3 wa wizi wa pikipiki  ambao ni Hamisi Juma 37 mkazi wa Olmatejoo, Isiaka Islam22 mkazi wa majengo moshi, na Hassan Mushi mkazi wa majengo mkoani Kilimanjaro

Hata hivyo kutokana na matukio hayo jeshi la polisi mkoani ARUSHA limewataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kutoa taarifa sahii ili kuweza kuendelea kuimarisha usalama

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

MBUNGE JAGUAR WA KENYA ALIYETISHIA KUWAFURUSHA WATANZANIA AKAMATWA

Maafisa wa polisi nchini Kenya wamemkamata mbunge wa jimbo la Starehe anayedaiwa kutoa kauli za chuki dhidi ya wafanyabiashara

Read More...

MANCHESTER CITY, YAMTOA KAFARA DANILO

. . Klabu ya Manchester City, ipo tayari kutoa kiasi cha paundi milioni 44 na beki wao wa pembeni

Read More...

TOTTENHAM MBIONI KUMSAJILI KIUNGO KUTOKA LYON.

. . Klabu ya Tottenham, imekubali kutoa kitita cha kiasi cha paundi milioni 62 kumsajili kiungo wa kati wa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu