Kamanda wa Polisi Arusha aahidi kukomesha madawa ya kulevya.

In Kitaifa

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha leo Mei 23, 2019 amefanya mahojiano katika kituo cha radio cha Radio 5 katika kipindi cha Goodmorning Tanzani na kuzungumza mambo kadha wa kadha hususani kwenye ulinzi na usalama Mkoani Arusha.

Hizi ni kauli alizozitoa kamanda katika mahojiano hayo.

“Huwezi ukawatendea haki watu kama huna hofu ya Mungu tunapeleleza kesi za mabilioni ya pesa na tunapata vishawishi lakini Makamanda tunahofu ya Mungu”.

“Mapambano ya dawa za kulevya hatutaangalia Chama cha Mtu hatutaangalia dini ya mtu hatuta angalia wadhifa wa mtu tutakukamata tu, tutapigana mpaka tone la mwisho mimi huwa sikubali kushindwa, vita hii ya madawa ya kulevya tutaishinda”.

“Ugoro sio madawa ya kulevya sema kuna wajanja, nikiwa jeshishini nikua mpelelezi kuna watu wajanjawajanja wanabadili dawa za kulevya wakidai ni ugoro”.

“Katika majeshi yenye vifaa vya kisasa Africa Tanzania ni ya kwanza, kwa umoja wetu tutaishinda hii vita na Arusha itakua Geneva kwelikweli. “Jonathan Shana

“Gari zetu zipo full tank hatuna tena tatizo la mafuta nyie tupeni taarifa tu, kuna madereva daladala wanawatoza pesa nyingi kwenye ruti fupi”.

Tukisema tii sheria bila shuruti ni utashi wa mtu, mtu ufate sheria bila kushurutishwa kupigwa virungu, unaenda kwenye maandamano unaambiwa acha huachi hadi utandikwe mabomu upigwe risasi ndio uache.

“Lockup hazijai hatuwezi kushindwa kutekeleza wajibu wetu wanachopaswa wananchi ni kutii bila shuruti.hakuna kitu kinachoishinda Serikali hasa serikali hii ya awamu ya tano thubutu.” J

“Wimbi la Watoto wa mitaani ni jukumu la Halmashauri zetu kuwatafutia mahali pakuishi au kuwasaidia malazi, nasisi tupo tayari kuwasaidiana na halmashauri watakapotuitaji.”

“Swala la Dada poa limekua na majina mengi wengine wanaita malaya, changudoa, swala hili bado lipo na mimi huwa napita naona, nadhani jukumu hili pia linawahusu halmashauri wajaribu kukaa nao watafute kazi nyingine.”

“Tumshukuru Rais Magufuli kwa maelekezo yao kufungua maduka ya kuuza madini lakini litawasaidia sana wachimbaji wa madini kutotapeliwa niwahakikishie wachimbaji kutotapeliwa”.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Miss Tanzania Mikononi mwa Waziri Mkuu

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemtaka mshindi wa shindano la urembo Tanzania (Miss Tanzania) kwa mwaka 2019 Sylivia Bebwa, kuhakikisha

Read More...

Magufuli ampandisha cheo Brigedia Jenerali Charles Mbuge.

Rais Magufuli amemteua Brigedia Jenerali Charles Mbuge kuwa Mkuu wa JKT. Mbuge anachukua nafasi Meja Jenerali Martin Busungu ambaye

Read More...

SOKA LA KIMATAIFA NA FUNUNU ZAKE.

Juventus imekataa kumuuza winga Douglas Costa 28 licha ya Man United kuwa na hamu ya kumsajili baada ya mkufunzi

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu