Kampeni ya uasi wa kiraia yazinduliwa sudan.

In Kimataifa

Watu zaidi ya 60 wauawa katika maandamano yanayodai utawala wa kiraia nchini Sudan, watu wanne wameuawa jana wakati vikosi vya usalama viliingilia kati kutuliza kampeni ya uasi wa kiraia iliyozinduliwa jana.

Waandamanaji waliweka vizuizi barabarani mjini Khartoum, huku masoko na maduka yakifungwa katika miji mingine nchini humo. Kamati ya madaktari inayohusishwa na waandamanaji ilisema watu wawili waliuawa katika makabiliano ya mji mkuu, wakati wengine wawili waliuawa katika mji wa Omdurman unaopatikana upande wa pili wa Mto Nile.

Wakati huo huo, mwanaharakati wa haki za wanawake nchini Sudan Nahid Jabrallah ameiambia DW kuwa matukio mengi ya ubakaji wa wanawake yameripotiwa wakati vikosi vya usalama vilipoingilia kati kuyavunja maandamano ya mjini Khartoum ya kulitaka jeshi likabidhi madaraka kwa utawala wa kiraia.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Miss Tanzania Mikononi mwa Waziri Mkuu

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemtaka mshindi wa shindano la urembo Tanzania (Miss Tanzania) kwa mwaka 2019 Sylivia Bebwa, kuhakikisha

Read More...

Magufuli ampandisha cheo Brigedia Jenerali Charles Mbuge.

Rais Magufuli amemteua Brigedia Jenerali Charles Mbuge kuwa Mkuu wa JKT. Mbuge anachukua nafasi Meja Jenerali Martin Busungu ambaye

Read More...

SOKA LA KIMATAIFA NA FUNUNU ZAKE.

Juventus imekataa kumuuza winga Douglas Costa 28 licha ya Man United kuwa na hamu ya kumsajili baada ya mkufunzi

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu