Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ametaka kuongezwa kwa juhudi katika mapambano dhidi ya magonjwa duniani.
Akizungumza mwishoni mwa Kongamano la Afya Duniani lililoandaliwa mjini Berlin, Merkel amesema afya ni jukumu la kila mmoja.
Kansela huyo ambaye amezungumza kwa kulenga mripuko wa Ebola uliotokea nchini Congo miezi kadhaa iliyopita amedai kuwa magonjwa ya kuambukiza kama hayo huenda yakaathiri usalama na ustawi wa kanda nzima.
Amesema mfano kama huo unaonyesha wazi kwa nini afya ni jambo linalohitaji ushirikiano wa dharura kwa ajili ya kuwepo kwa ustawi wa kudumu kwa kila mmoja duniani.