Katibu tawala wa Mkoa wa Arusha asema serikali ina wajibu wa Kuhudumia watoto cha SOS.

In Kitaifa

Katibu tawala wa Mkoa wa Arusha Richard Kuitega amesema serikali ina wajibu wa kuanza kusaidia kituo cha Kuhudumia watoto cha SOS,ambacho kilikuwa kinahudumiwa na wafadhali kutoka nje ya nchi.

Akizungumza wakati alipotembelea taasisi inayohudumia watoto yatima ijulikanayo kama SOS children iliyopo Ngaramtoni mkoani Arusha  katibu huyo, amesema serikali ina Jukumu la kutoa ushirikiano ili kuweza kuendeleza miradi mbalimbali kwa manufaa ya Wananchi

Kuitega  amesema kuwa  serikali itaanza kwa kutoa wataalamu watakao toa huduma kituoni hapo  kama vile walimu ili kuhakikisha kuwa wanapunguza baadhi ya changamoto.

Kwa upande wake Mkurugenzi  wa Shirika hilo Fransis Msolo amesema kituo hicho kilikuwa chini ya wafadhili ,ambao kwa sasa wanajitoa hivyo ipo haja ya serikali kupandisha hadhi kituo hicho ili kiweze kutoa huduma ndani ya  Jamii.

Halikadhalika taasisi hiyo imeweza kutunza watoto Elfu moja 1000 ambapo wengine amefika  hadi elimu ya Juu ya Vyuo Vikuu na kuweza kujiendeleza Kimaisha.

 

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu