Kauli aliyetoa Mh Mbowe baada ya Lissu kupoteza Ubunge.

In Kitaifa

Kauli aliyetoa Mh Mbowe baada ya Lissu kupoteza Ubunge.

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania cha Chadema, Freeman Mbowe amesema uamuzi wa Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai la kutangaza nafasi kiti cha ubunge wa Singida Mashariki kilichokuwa kikikaliwa na Tundu Lissu kiko wazi halijawatikisa wala kuwakatisha tamaa bali kuzidi kuimarisha dhamira yao ya kushika dola.

Mbowe ambaye ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni Tanzania alitoa msimamo huo wa chama leo Jumamosi Juni 29, 2019 wakati wa kikao cha ndani kilichofanyika jana Kanda ya Nyasa.

Alisema chama hicho kipo tayari hata kupoteza viti vyake vyote lakini hakitaacha kufanya kazi kwa ajili ya wananchi hivyo amewataka wanachama wa chama hicho kutokuwa na mioyo ya visasi.

“Yaani Spika leo anamfukuza ubunge Tundu Lissu anafikiri tutalia, tunamwambia mheshimiwa spika wacha Lissu chukua viti vyote hivi, nani ana shida na ubunge, tuna shida na wananchi,” alisema Mbowe

“Wanatupa sababu zaidi za kufanya kazi vitu kama hivi haviwezi kutukatisha tamaa, vinatuimarisha katika dhamira yetu, tunafanyiwa uonevu mwingi ndani ya bunge, tunafanyiwa visa vingi. Hivi visa havituvunji moyo, vinatuimarisha.”

Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai alisema, “Hasira ya kufukuza wabunge wetu, hasira ya kutoheshimu mawazo yetu, hasira ya kuondoa michango yetu tutaimaliza kwa kupeleka wabunge wengi, kuondoa wingi wa CCM ndani ya bunge na kuiongoza serikali ya nchi hii.”

Mbowe alilalamikia pia Kamati ya Haki, Kinga na Maadili ya Bunge kwa kuwashughulikia wabunge wa upinzani pekee huku ikionekana kushindwa kuwagusa wabunge wa CCM.

“Uonevu huu wanaotufanyia, hatuna sababu ya kuwatukana, tunacheka lakini dhamira ndani ya mioyo yetu inaimarishwa sana kila mbunge wetu angesimama kueleza anafanyiwa nini sijui ingekuwaje,” alisema

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

David Luiz kuitangaza Rwanda Kimataifa.

Mchezaji wa klabu ya Arsenal, David Luiz ameahidi kuitangaza Rwanda kimataifa kwenye sekta ya utalii kwa marafiki zake wanaoishi

Read More...

Rekodi yawekwa na Kipchoge kutoka Kenya

Eliud Kipchoge amekuwa Mwanariadha wa kwanza katika historia ya mbio za marathon kukimbia kilomita 42 kwa muda wa chini

Read More...

Habinder Seth aandika barua kwa DPP kukiri makosa yake.

Habinder Seth, anayekabiliwa na makosa ya Uhujumu Uchumi amemuandikia barua Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) kukiri makosa yake na

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu