Kauli ya Waziri Jafo Baada Ya CHADEMA Kutangaza Kujitoa Uchaguzi Serikali za Mitaa.

In Kitaifa
Baada  ya Chadema kutangaza kutoshiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa, Waziri wa Tamisemi, Seleman Jafo amesema uamuzi huo unawanyima fursa wagombea wa chama hicho waliopitishwa, waliokata rufaa kupinga kuenguliwa.
Jana  jioni Alhamisi Novemba 7, 2019 mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema chama hicho kimejitoa na hakitashiriki uchaguzi wa serikali za mitaa kwa kuwa ni kuhalalisha ubatili, akibainisha kuwa takribani asilimia 85 ya wagombea wao nchi nzima wameenguliwa.
Katika maelezo yake Jafo amesema; “Nimesikia kuwa Chama kimojawapo kimejitoa kwenye Uchaguzi, ninachoweza kusema ni kuwa hawajawatendea haki Wananchi wa chini kwa sababu baadhi yao walishateuliwa na wengine wameshawasilisha malalamiko yao kwenye Kamati za Rufaa na tayari baadhi ya Kamati za Rufaa zimeshaanza kutoa maamuzi juu ya rufaa hizo.

“Mtazamo wangu maamuzi hayo yatawanyima haki na kuwadhulumu wananchi wa chini haki yao ya kugombea na kuongoza Serikali za Mitaa ambao baadhi yao wameshateuliwa na wengine wanasubrii rufaa zao”

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu