Wizara ya Afya nchini Kenya imezindua Teknolojia ya kutumia
Roboti ili kupambana na janga la virusi vya Corona na hatari
yake kwa wafanyakazi wa Afya kwa wagonjwa wa Covidi 19
walio chini ya uangalizi wao.
Mutay Kagwe ambaye ni waziri wa Afya amesema kuwa roboti
hizo zitatumika katika hosipitali kuu ya rufaa nchini humo,
hospitali ya kitaifa ya Kenyata na uwanja wa ndege wa Jomo
Kenyata.
Roboti hizo tatu zilizopewa majina ya Jasiri,Shujaa na Tumani
zinatarajiwa kusaidia katika uchunguzi wa hali ya joto,kuuwa
vijidudu,mawasiliano ya ujumbe wa Afya na ukusanyaji wa
data.
