KESI YA KUPINGA SHERIA YA VYAMA VYA SIASA YASIKILIZWA LEO ARUSHA.

In Kitaifa

Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki iliyopo Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki mjini Arusha, leo Novemba 6, 2019 imesikiliza maombi madogo ya kesi Na.2/2019 iliyofunguliwa na Mwenyekiti wa (CHADEMA) Taifa Freeman Mbowe pamoja na Viongozi wengine 4 wa vyama vya Siasa Nchini kupinga sheria ya vyama vya siasa.

Maombi yaliyosikilizwa leo ni maombi ya kutaka Mahakama isimamishe matumizi ya sheria Na.1 ya vyama vya Siasa ambayo imetungwa mwaka 2019  hadi kesi ya msingi Namba 3/20 itakaposikilizwa.

Kesi hiyo ilihudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu wa (CHADEMA) Zanzibar Salim Mwalimu, Makamu wa Kwanza wa Rais Mstaafu na kiongozi wa ACT Maalim Seif Sharif pamoja na Katibu wa (CHADEMA) Kanda ya Kaskazini Amani Golugwa.

Mahakama imesikiliza hoja za pande zote mbili na itatoa majibu yake pindi itakapowataarifu.

 

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Mgombea urais wa chama tawala Burundi atangazwa mshindi kwa kupata asilimia 68.7

Mgombea urais wa chama tawala nchini Burundi Evariste Ndayishimiye ametangazwa mshindi leo kwenye kinyang’anyiro hicho ambacho kimedaiwa kukumbwa

Read More...

Watu 7 Wanaodhaniwa Kuwa Majambazi Wauawa Dar es Salaam

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kuwaua majambazi saba na kufanikiwa kukamata silaha ndogo Bastola

Read More...

Watanzania watakiwa kucheki afya zao na kufuata ushauri wa daktari.

Watanzania wametakiwa kuwa na mazoea ya kwenda vituo vya afya kucheki afya zao na kuacha dhana ya kutumia

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu