Kichaa awakatakata Watoto kwa panga.

In Kitaifa

Watoto sita wameuawa na wanne wamejeruhiwa kwa kucharangwa kwa panga  na mwanamke aliyejulikana kwa jina la Nana Maganga 35  anayedaiwa kuwa na matatizo ya akili. .

Hata hivyo mwanamke huyo ambaye ni  mkazi wa kijiji cha Luzuko kata ya Mizibaziba wilaya ya Nzega Mkoani Tabora, naye aliuawa wakati akidhibitiwa na wananchi.

Aidha imefafanuliwa kuwa kati ya watoto hao sita, watano  ni wa kwake mwenyewe na mmoja ni mtoto wa kaka yake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Emmanuel Nley akithibitisha kutokea kwa mauaji ya watu hao, amesema kuwa  Nana kutokana na tatizo lake la ugonjwa wa akili alikwenda kwa mganga wa jadi ambaye ni shemeji yake kwa lengo la kupatiwa matibabu ndipo mkasa huo wa kuwakata kwa panga watoto wake ambao alikuwa amelala nao katika chumba kimoja ulipotokea.

Kamanda Nley amesema kuwa waliomdhibiti Nana wakati akitekeleza mauaji hayo akiwemo shemeji yake, walidai walimdhibiti kwa kumfunga kamba ambapo baadaye mwenyewe alikunywa sumu na kupoteza maisha.

Amesema jeshi la polisi linawashikilia watu watano akiwepo mume wa Nana na mganga wa jadi kwa tuhuma za kumuua Nana na kuongeza kuwa upelelezi wa tukio hilo unaendelea ili kujua nini chanzo cha mauaji hayo ambayo yamesababisha vifo vya watoto wadogo wasiokuwa na hatia.

Amewataja watoto hao kuwa ni pamoja na Pala Massanja mwenye umri wa miaka 3, Shija Dotto 2, Nyawele Dotto2, Sida Dotto5 , Kulwa Dotto 4 Dotto Dotto, 4  pamoja na Nana.

Aidha amewataja watoto wengine waliojeruhiwa katika tukio hilo kuwa ni Kundi Dotto, Nembwa Dotto, Milembe Massanja pamoja na Mwashi Massanja.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

MBUNGE JAGUAR WA KENYA ALIYETISHIA KUWAFURUSHA WATANZANIA AKAMATWA

Maafisa wa polisi nchini Kenya wamemkamata mbunge wa jimbo la Starehe anayedaiwa kutoa kauli za chuki dhidi ya wafanyabiashara

Read More...

MANCHESTER CITY, YAMTOA KAFARA DANILO

. . Klabu ya Manchester City, ipo tayari kutoa kiasi cha paundi milioni 44 na beki wao wa pembeni

Read More...

TOTTENHAM MBIONI KUMSAJILI KIUNGO KUTOKA LYON.

. . Klabu ya Tottenham, imekubali kutoa kitita cha kiasi cha paundi milioni 62 kumsajili kiungo wa kati wa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu