Kigwangala afikishwa Muhimbili, Rais Magufuli ampokea.

In Afya

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amempokea Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla amewasili katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa matibabu zaidi.

Ndege iliyombeba waziri huyo ilitua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 12 jioni na kupokelewa na Rais John Pombe Magufuli.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Dk Mpoki Ulisubisya na mkurugenzi mtendaji wa Muhimbili, Profesa Lawrence Museru pamoja na jopo  la madaktari wamempokea Dk Kigwangalla katika  kitengo cha magonjwa ya dharura Muhimbili.

Dtk Kigwangalla amepata ajali leo Jumamosi Agosti 4, 2018 eneo la Magugu mkoani Manyara na kupata majeraha sehemu mbalimbali mwilini

Awali,  waziri huyo alipatiwa matibabu katika kituo cha afya cha Magugu na kuhamishiwa hospitali ya Arusha Lutheran Medical Center kwa helkopta.

Katika ajali hiyo ofisa habari wa wizara hiyo, Hamza Temba amefariki dunia.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Majeshi ya Marekani yauwa raia Somalia

Majeshi ya Marekani yanayoendesha mashambulizi ya angani nchini Somalia dhidi ya ngome za wapiganaji wa Al Shabab nchini humo

Read More...

Idai yapoteza makazi ya watu 400,000.

Shirika la Msalaba Mwekundu linakadiria kuwa watu 400,000 wamepoteza makaazi yao nchini Msumbiji kutokana na Kimbunga Idai kilichoipiga nchi

Read More...

Baa la njaa kuikumba Kenya.

Zaidi ya watu milioni 1.5 nchini Kenya wako katika hatari ya kukabiliwa na baa la njaa kufuatia kutokuwepo kwa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu