Kilimanjaro Stars na Zanzibar wapwangwa kundi moja

In Kitaifa, Michezo

TIMU ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars imepangwa katika Kundi C pamoja na Zanzibar, Kenya na Djibouti katika Mashindano ya Kombe la Chalenji kwa timu za wanaume.
Ratiba ya mashindano hayo, ambayo yatafanyika Kampala, Uganda kuanzia Desemba 7-18, ilipangwa jana jijini Dar es Salaam na kutangazwa na Katibu Mkuu wa Baraza la Soka la Afrika Mashariki (Cecafa), Nicolaus Musonye.

Hii ni mara ya pili kwa Tanzania Bara kupangwa pamoja na Zanzibar, kwani katika michuano ya wanawake ya Cecafa inayomalizika leo jijini Dar es Salaam, katika hatua ya makundi, timu hizo zilikuwa pamoja katika Kundi A, lakini Zanzibar ilitolewa mapema.

Kwa mujibu wa ratiba hiyo, Kundi A linaundwa na wenyeji Uganda ambao watakuwa pamoja na Ethiopia, Eritrea na Burundi wakati Kundi B linaundwa na timu mualikwa ya DR Congo, Sudan Kusini, Ethiopia, Burundi na Sudan.
Mbali na ratiba hiyo ya wakubwa, Cecafa pia jana ilipanga ratiba ya makundi kwa timu za wasichana wenye umri chini ya miaka 17, ambayo mashindano yake yatafanyikia Jinja, Uganda pia.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu