Kim Jong un akubali kuangamiza silaha za kinyuklia Korea

In Kimataifa

Vyombo vya habari vya Korea kazkazini vimekuwa vikisifia mkutano wa jana uliokuwa wa kihistoria kwa namna nyingi -ambapo miongoni mwa matukio mengineyo kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong Un walikubaliana kufanya kazi pamoja na rais wa Korea kusini Moon Jae-in, katika kile walichosema ni kuhakikisha hamna silaha za kinunyuklia katika rasi nzima ya Korea.

Runinga ya serikali imemlimbikizia sifa na kumpa hongera Kim Jong-un kwa kufanikisha hayo wakisema ni kutokana na upendo wake kwa raia wake na kutaka pia nchi hiyo iweze kujitegemea .

Msimamo huo ni tofauti na jinsi vyombo vya habari vya Korea kusini walivyouchambua mkutano huo.

Rais Kim Jong un
Rais Kim Jong un

Wadadisi wa maswala ya kisiasa wanasema si rahisi kutabiri azma ya baadaye ya Kim Jong Un hasa swala la iwapo kweli atatupilia mbali miradi yake ya kinyuklia, wakihoji kuwa hakutoa hakikisho lolote linaloweza kuaminika.

Rais wa Marekani Donald Trump amesema ataendelea kuishinikiza Korea kaskazini kuachana na miradi yake ya kinyuklia licha ya mafanikio makubwa ya mkutano wa jana baina ya viongozi wa Korea ya Kusini na Kim Jong Un wa Korea kaskazini.

Trump pia amesisitiza azma yake ya kukutana na kiongozi huyo wa Korea kaskazini kwa matumaini kwamba ataweza kumshawishi asiendelee kujilimbikizia silaha hizo hatari.

Katika mkutano huo wa jana uliokuwa wa kihistoria kwa namna nyingi Kim Jong un alikubaliana kufanya kazi pamoja na rais wa Korea kusini Moon Jae-in, katika kuhakikisha hamna silaha kinyuklia katika rasi nzima ya Korea.

Hata hivyo wadadisi wa maswala ya kisiasa wanasema si rahisi kutabiri azma ya baadaye ya Kim Jong Un hasa swala la iwapo kweli atatupilia mbali miradi yake ya kinyuklia.

Korea Kazkazini imewekewa vikwazo vya kiuchumi chungu nzima kutokana na kukataa kwake kusitisha miradi hiyo ya kinyuklia ambayo imekuwa ikiwatia wasiwasi jirani zake , Korea Kusini, Japan na washirika wao wa karibu Marekani – wanaosema inawahatarishia usalama wao.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu