King Kiba:Nimeleta kinywaji kuwapa nguvu ya kufanya kazi.

In Burudani

Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini anayefanya vizuri katika tasnia hiyo, Ali Kiba maarufu kama King Kiba amesema aliamua kutengeneza kinywaji cha ”Energy Drink” cha Mofaya yaani kinywaji cha kuleta nguvu kutokana na kwamba watanzania wengi wanafanya kazi na ili kuendana na kauli mbiu ya Rais John Pombe Magufuli ya hapa kazi tu hivyo kinywaji hiko kitawapa nguvu ya kufanya kazi kwa ubora zaidi.

”Mimi nimeona nilete kinywaji kuwapa nguvu kufanya kazi zaidi na kuamsha akili zetu ili kuleta ufanisi zaidi” amesema Alikiba.

Ameongezea kuwa wazo la Energy Drink limekuja kutokana na kazi yake ya muziki kwani mara zote kabla ya kupanda katika stage kufanya show hutumia kinywaji cha Energy Drink ili kumpa nguvu ya kufanya vizuri, na kutokea hapo aliona umuhimu wa kuwa na kinywaji chake mwenyewe ambacho kitatumiwa na watu wengi zaidi.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

MO apatikana, atelekezwa na watekaji.

Habari zilizotufikia hivi punde zinasema Bilionea/Mfanyabiashara maarufu nchini Tanzania, Mohammed Dewji ‘Mo’  aliyetekwa na watu wasiojulikana Oktoba 11,2018 amepatikana

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu