Kitendo cha Kutikisa gesi ili kujua kama ipo ni hatari, husababisha mlipuko wa moto.

In Kitaifa
Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini Kamishina Jenerali Thobias Andengenye ameliagiza Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, kuendelea kufanya ukaguzi wa kinga na tahadhari ya moto kwa shule zote za sekondari za mabweni nchini kujiridhisha ikiwa vigezo vimezingatiwa, kwa lengo la kuepusha majanga ya moto yanayogharimu maisha ya watu na mali. 
Andengenye ametoa maagizo hayo Juni 19, 2019 Mkoani Simiyu wakati akizungumza na wanafunzi wa baadhi ya shule za msingi na sekondari za Mjini Bariadi katika shule ya sekondari Simiyu, katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi. 
Akizungumza na wanafunzi Kamishina Jenerali Thobias Andengenye amesema kumekuwa na matukio ya moto katika shule kadhaa za bweni ambayo yameleta athari mbalimbali ikiwa ni pamoja na kusababisha vifo kwa wanafunzi, kuteketea kwa mali, hivyo jeshi la zimamoto na uokoaji linaendelea kuweka mikakati ya kukabiliana na majanga hayo. 
Amesema mikakati hiyo ni pamoja na kusogeza huduma za zimamoto karibu na wananchi kufanya ukaguzi wa tahadhari na kinga ya moto katika majengo, kusoma ramani za majengo na kuanzisha klabu za zimamoto katika shule, ili kuwajengea wanafunzi uwezo wa kujua vitu vya kufanya na vya kuepuka na uwezo wa kukabili moto katika hatua za awali na kuuzima. 
Katika hatua nyingine Andengenye amewataka wamiliki wa shule kuzingatia ushauri wa kitaalam unaotolewa na wataalam wakati wa ukaguzi juu ya namna ya kufanya mabweni , madarasa na ofisi ziwe salama kwa kuwasilisha michoro ya majengo hayo katika Ofisi za Zimamoto ili ushauri wa kitaalam uweze kutolewa. 
“Niwaombe wanaomiliki shule wazingatie ushauri wa kitaalam unaotolewa, wazingatie ujenzi unaofuata ushauri wa kitaalaam kwa kuwasilisha michoro kama wanataka kujenga mabweni, kuongeza madarasa au kuongeza vyumba vya ofisi basi wazingatie ushauri ili majengo yanayojengwa yawe salama zaidi” alisema. 
Aidha, amewaasa wananchi kuacha kuweka mitungi ya gesi ndani na kutikisa mitungi ya gesi kama njia ya kufahamu kiasi cha gesi kilichopo; kwa kuwa kunaweza kusababisha moto na kushauri kuwa njia sahihi ya kupima kiasi cha gesi katika mtungi ni kuweka mtungi katika maji, ambapo baada ya kuutoa sehemu isiyo na gesi itaonekana kuwa kavu. 

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu