Kocha wa Liverpool awaonya Real Madrid

In Michezo

Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp ameitahadharisha klabu ya Real Madrid kuelekea mchezo wao wa fainali wa klabu bingwa barani Ulaya hapo kesho Mei 26, 2018.

Klopp amesema kuwa anafahamu fika klabu yake haina uwezo mkubwa kulinganisha na wapinzani wao Real Madrid lakini hiyo siyo sababu kwa Madrid kuwapeza kwani wana historia nzuri kwenye mechi kubwa.

Sisi ni Liverpool sio timu mzuri pekee hata hao (Real Madrid) lakini tuna vina saba vya  kufanya vizuri kwenye mechi kubwa. Hakuna aliyejua kama tutafika hapa lakini leo hii tupo hapa na hii ni kwa sababu sisi ni Liverpool.“amesema Jugen Klopp kwenye mkutano wake na Waandishi wa Habari jioni ya leo mjini Kiev, Ukraine.

Wengine waliotoa mitazamo yao ni wachezaji wa Liverpool, Van Dijk na Nahodha Jordan Brian Henderson ambao wote wamekiri kuwa gemu ni nzito ila wataushangaza ulimwengu.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

MO apatikana, atelekezwa na watekaji.

Habari zilizotufikia hivi punde zinasema Bilionea/Mfanyabiashara maarufu nchini Tanzania, Mohammed Dewji ‘Mo’  aliyetekwa na watu wasiojulikana Oktoba 11,2018 amepatikana

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu