Kocha wa Simba afunguka baada ya kupokea kipigo.

In Michezo

BAADA ya Simba kupoteza nafasi ya kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya nusu fainali, Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amesema nguvu zake kubwa anaziwekeza kwenye ligi.

Simba ilipoteza mchezo wake wa pili mbele ya TP Mazembe kwa kufungwa mabao 4-1 hali iliyofanya ndoto yao ya kusonga mbele kuishia Congo.

Aussems amesema kuwa amejifunza mengi na kugundua kwamba kikosi chake kina uwezo mkubwa hivyo makosa aliyofanya atayafanyia kazi ila kwa sasa nguvu ni kwenye ligi.

“Tumepoteza nafasi yetu ya kusonga mbele ila hakuna cha kujutia sana kwa kuwa ushindani ulikuwa mkubwa nasi tumepambana, haikuwa bahati yetu sasa tunaweka akili yetu kwenye ligi.

“Tuna michezo mingi ya kucheza na wachezaji tayari wameshaanza kuona namna ushindani ulivyo na mashindano ya kimataifa yanavyokwenda nina amini msimu ujao tutakuwa na nafasi nzuri zaidi tukirejea,” amesema Aussems.

Kikosi cha Simba leo tayari kimefika salama jijini Tanga na jioni kitaanza mazoezi kujiandaa kuwakabili Coastal Union siku ya Jumatano.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

MBUNGE JAGUAR WA KENYA ALIYETISHIA KUWAFURUSHA WATANZANIA AKAMATWA

Maafisa wa polisi nchini Kenya wamemkamata mbunge wa jimbo la Starehe anayedaiwa kutoa kauli za chuki dhidi ya wafanyabiashara

Read More...

MANCHESTER CITY, YAMTOA KAFARA DANILO

. . Klabu ya Manchester City, ipo tayari kutoa kiasi cha paundi milioni 44 na beki wao wa pembeni

Read More...

TOTTENHAM MBIONI KUMSAJILI KIUNGO KUTOKA LYON.

. . Klabu ya Tottenham, imekubali kutoa kitita cha kiasi cha paundi milioni 62 kumsajili kiungo wa kati wa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu