Kocha wa simba kuwaboreshea mikataba wachezaji wake.

In Michezo

KOCHA Mkuu wa Simba Mbelgiji, Patrick Aussems amepanga kuwaboreshea mikataba baadhi ya wachezaji wake wazawa kwa sharti awe amecheza nusu ya mechi za Ligi Kuu Bara na michuano mingine waliyoshiriki.

Kati ya wachezaji waliopendekezwa kuboreshewa mikataba yao ni viungo wa timu hiyo, Said Ndemla na Mohamed Ibrahim ‘Mo’ ambao wote hivi karibuni walikuwa wanatajwa kuwaniwa vikali na Yanga.

Ndemla yeye mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu huku Mo akibakisha mwaka mmoja ambaye alikuwa anatajwa kutolewa kwa mkopo.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumamosi, kocha huyo amefi kia hatua ya kuboresha mikataba ya wachezaji hao kutokana na kutovutiwa na viwango vya wachezaji wazawa.

Mtoa taarifa huyo alisema, kama kungekuwepo na wachezaji wazawa wenye uwezo kushinda alionao hivi sasa, basi angefanya usajili hivyo amependekeza kuendelea na wachezaji hao katika msimu ujao.

“Ukiangalia viwango vya wachezaji wazawa waliopo kwenye timu nyingine hakuna waliowazidi waliopo Simba, hiyo ndiyo sababu kubwa inayomfanya kocha apendekeze kubaki nao na waboreshewe mikataba kwa wale ambao mikataba yao inatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu.

“Kocha anataka mchezaji mpya atakayesajiliwa Simba awe na uwezo mkubwa utakaompa changamoto mchezaji atakayemkuta siyo asajiliwe halafu akae benchi,” alisema sosi huyo.

Alipotafutwa Aussems alisema: “Tangu msimu huu wa ligi umeanza sijaona mchezaji mzawa aliyenivutia nimsajili. Nimependekeza kwa uongozi kuwaboreshea baadhi ya wachezaji mikataba yao kwa wale ambao inamalizika mwishoni mwa msimu.”

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Baraka da Prince sasa kufunga ndoa na Naj

Msanii wa Bongo fleva Baraka de Prince amebainsha wazi kufunga ndoa mwaka huu na mpenzi wake Naj. Minong’ono ilikua

Read More...

Ajibuawataka Simba watulize boli, msimu ni wao

Nyota wa Simba, Ibrahim Ajibu amesema kuwa mashabiki wa Simba watulie watakubali mziki wake kwani amejipanga kufanya maajabu. Ajibu

Read More...

Waziri Mkuu kuzindua Daftari la kudumu la kupiga kura.

Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC Dkt Athumani Kihamia, amesema zoezi la uandikishaji wa daftari la Kupiga

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu