Koffi Olomide jela miaka 2 kwa ubakaji.

In Burudani

Koffi Olomidé,  nyota wa muziki Afrika , amekutwa na hatia kwa ubakaji wa mmoja wa  wanengeuaji wake alipokuwa na miaka 15.

Amehukumiwa miaka miwili gerezani na mahakama ya Ufaransa akiwa hayupo, baada ya kushindwa kufika mahakamani.

Uamuzi huo una maana kwamba nyota huyo wa Congo atakamatwa iwapo atatekeleza uhalifu mwingine,

Olomidé, mwenye umri wa miaka 62, aliagizwa alipe Euro 5,000 kwa madhara aliyomsababishia mnenguaje wake huyo wa zamani.

Mahakama ya Nanterre, nje ya mji mkuu Paris, pia ilimuagiza alipe faini ya kiwango sawa kwa kuwasaidia wanawake watatu wengine kuingia nchini Ufaransa kwa njia haramu.

Wakili wa Olomidé amepongeza uamuzi huo na kuutaja kuwa ushindi, akiwarifu waandishi habari kwamba uamuzi huo utachangia kuondolewa waranti wa kimataifa wa kumkamata.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

MBUNGE JAGUAR WA KENYA ALIYETISHIA KUWAFURUSHA WATANZANIA AKAMATWA

Maafisa wa polisi nchini Kenya wamemkamata mbunge wa jimbo la Starehe anayedaiwa kutoa kauli za chuki dhidi ya wafanyabiashara

Read More...

MANCHESTER CITY, YAMTOA KAFARA DANILO

. . Klabu ya Manchester City, ipo tayari kutoa kiasi cha paundi milioni 44 na beki wao wa pembeni

Read More...

TOTTENHAM MBIONI KUMSAJILI KIUNGO KUTOKA LYON.

. . Klabu ya Tottenham, imekubali kutoa kitita cha kiasi cha paundi milioni 62 kumsajili kiungo wa kati wa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu