Korea Kaskazini ipo tayari kukutana na Trump wakati wowote.

In Kimataifa

Korea Kaskazini imeelezea kusikitishwa kwake na hatua ya rais Donald Trump kujitoa katika mazungumzo yaliyopangwa kufanyika juni 12 huko Singapore.

Kwa mujibu wa mashirika ya habari nchini humo, uamuzi huu umekuwa kinyume na matarajio ya dunia.

Inadaiwa kuwa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-Un alikuwa amefanya jitihada zote katika maandalizi ya mkutano huo na kwamba Pyongyang ilikuwa tayari kuhakikisha tofauti zilizopo kati ya taifa lake na Marekani zinasuluhishwa kwa namna yoyote na popote, lakini Trump mwenyewe amesema uwezekano wa kufanyika mazungumzo hayo bado upo.

Taarifa hizo pia zimeleta mshtuko kwa jumuiya ya kimataifa, ambapo katibu mkuu wa umoja wa mataifa Antonio Guterres, ameelezea kuguswa kwake na hatua hiyo ya Marekani huku naye rais wa Korea Kusini Moon Jae-In akitoa wito kuwepo kwa mkutano wa dharura wa viongozi wa juu wa usalama kuhusiana na suala hilo.

kutano huu ungejadili namna ya uondoaji wa silaha za nyuklia katika rasi ya Korea kufuatia mkutano wa Korea zote mbili uliofanyika mwezi April mwaka huu.

Hata hivyo yapo baadhi ya mambo yanayotajwa kama dosari zilizo jionyesha kuelekea mazungumzo hayo na hasa kauli za kushinikiza msimamo wake ndani ya barua aliyomuandikia kiongozi wa Korea Kaskazini baada ya kuwa na mazungumzo na rais wa Korea kusini Moon.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu