Kwa mara ya kwanza shule ya sekondari ya Emboreet itaanza kuokea wanafunzi wa kidato cha tano kwa mwaka huu.

In Kitaifa

Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara ambayo haina shule ya kidato cha tano na sita, kwa mara ya kwanza shule ya sekondari ya Emboreet itaanza kupokea wanafunzi wa kidato cha tano kwa mwaka huu.

Mkuu wa wilaya ya Simanjiro mhandisi Zephania Chaula, akizungumza  kwenye kikao cha baraza la madiwani amesema wamejipanga shule hiyo ianze kupokea wanafunzi wa kidato cha tano, Julai mwaka huu.

Chaula amesema hadi hivi sasa shule ya sekondari Emboreet  ya kidato cha nne, imeboreshwa kwa ajili ya kupokea wanafunzi wa kidato cha tano, kwani awali wilaya ilikuwa haina shule ya kidato cha tano na sita.

Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Jackson Sipiti eck, mkurugenzi mtendaji Yefred Myenzi na madiwani, wametenga sh 12 milioni, kwa ajili ya matengenezo ya miundombinu ya shule hiyo.

Amesema diwani wa kata ya Emboreet, Christopher Kuya anastahili kupongezwa, kwa kusimamia kitendo cha shule hiyo kufanikiwa kuwa na hatua ya kidato cha tano na sita kwani ni maendeleo kwa Simanjiro

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu