Leteni Mbunge Wa Kupitisha Bajeti, Siyo Wa Kupinga Tu – Majaliwa

In Kitaifa, Siasa

MJUMBE wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Kassim Majaliwa amewataka wakazi wa Kilwa wamchague mbunge ambaye atakuwa tayari kupitisha bajeti na kuwaletea maendeleo.

“Msilete watu wa kukataa fedha, bali leteni mtu wa kukubali fedha zipitishwe ili mpate maendeleo,” amesema.


Ametoa wito huo leo (Alhamisi, Oktoba 22, 2020) wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na wakazi wa Ilulu Njianne katika kata ya Tingi na kata ya Kivinje kwenye mikutano iliyofanyika wilayani Kilwa, mkoani Lindi.

“Tanzania inahitaji watu makini na pale Bungeni siyo mahali pa viburudisho. Bunge linahitaji watu wa kuwasemea wananchi na siyo kuleta burudani wakati wengine wako kazini,” amesema.

Mheshimiwa Majaliwa leo yuko mkoani Lindi kumuombea kura mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Dkt. John Pombe Magufuli. Ametumia fursa hiyo kuwanadi wagombea ubunge wa majimbo ya Kilwa Kaskazini, Bw. Francis Ndulane na Kilwa Kusini, Bw. Ally Kasinge pamoja na wagombea udiwani wa kata za majimbo hayo kwa tiketi ya CCM.

“Mleteni mtu anayeweza kujenga hoja na kuitetea. Fedha zisipopitishwa maendeleo yenu hayawezi kuja kwa sababu hakuna mtu wa kuwasemea. Wana-Kilwa msiniangushe, Jumatano ijayo ikifika, chukua karatasi yako weka tiki kwa Dkt. Magufuli; kwa mbunge wa CCM na kwa diwani wa CCM.”

Aliwataka wakazi hao wawachague wagombea wa CCM kwa sababu chama hicho kina makada wazuri na kimewaandaa vizuri viongozi wake. “Kitendo cha Kamati Kuu kuwapa nafasi hawa waliopitishwa, hakikuwa na nia ya kumuonea mtu bali kuwapanga viongozi wake kulingana na majukumu.”

Mapema, mtia nia aliyeongoza kwenye kura za maoni katika jimbo la Kilwa Kaskazini, Bw. Murtaza Mangungu alipopewa nafasi ya kuwaombea kura wagombea wa CCM alitumia fursa hiyo kuwaonya watu wanaoweka maneno maneno dhidi yake.

“Wako watu ambao walitaka kusafiria nyota yangu. Wakati tunazindua kampeni, nilitamka kutoka moyoni mwangu, siyo kinywani tu, kwamba nitafanya kazi kuhakikisha Chama cha Mapinduzi kinashinda. Namuombea kura Dkt. Magufuli, namuombea kura kaka yangu Francis Ndulane na mgombea udiwani wa Tingi, Rajab Ngatanda,” alisema.

(mwisho)

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Tetesi za Soka Ulaya leo Alhamisi Septemba 23, 2021

Mshambuliaji wa Arsenal na Ufaransa Alexandre Lacazette, 30, hana hamu ya kusaini kandarasi mpya klabuni hapo. Mkataba wake wa

Read More...

Wanaharakati wa haki za binadamu wahoji hukumu dhidi ya Rusesabagina

 Makundi ya kutetea haki za binadamu barani Afrika yamelalamikia uamuzi wa mahakama kuu ya Rwanda ya kumfunga jela kwa miaka 25, Paul Rusesabagina ambaye alisifika sana kwenye filamu ya Hollywood ya Hotel Rwanda.  Mahakama hiyo Jumatatu ilisema kwamba imepata Rusesabagina pamoja na washukiwa wengine 20 na hatia ya

Read More...

LISSU NA WENZAKE WAFUTIWA KESI

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeifutia kesi ya uchochezi iliyokuwa inamkabili Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleao

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu