Lowassa avunja ukimya kuhusu tuhuma inayomkabili.

In Kitaifa
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa amesema hamtambui mwanamke aliyejitambulisha juzi kama binti yake aliyetelekezwa na kwamba hatapoteza muda kwenda kupimwa vinasaba (DNA), kama msichana huyo alivyotaka.
Kwa mujibu wa mazungumzo na Gazeti la Nipashe, Lowassa ambaye kwa sasa ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), alisema kuwa kinachofanyika kwenye zoezi hilo ni siasa.
Msichana huyo aliyejitambulisha kwa jina la Fatuma alijitokeza hadharani juzi katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na kudai kutelekezwa na Lowassa ambaye alisema ni baba yake, kwa kuambiwa na mama yake mzazi.
“Wewe unamwamini kweli huyo msichana? Angekuwa mwanangu kweli ningeshamchukua muda mrefu, kwanza wala simjui naona siasa zinaingizwa hapo,” alisema.
Alipoulizwa kama yuko tayari kupimwa DNA ili ukweli ujulikane, Lowassa alijibu “Kupima DNA huo ni upuuzi. Yaani nipoteze muda wangu kwenda kufanya upuuzi huo? Siko tayari.”
Msichana huyo ni miongoni mwa mamia ya wanawake waliojitokeza kuanzia Jumatatu kuitikia wito wa Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda.
Makonda alitaka wanawake waliotelekezewa watoto na waume zao wafike ofisini kwake kwa siku tatu kuanzia Jumatatu, kwa ajili ya kuzungumza na wanasheria, maofisa wa ustawi wa jamii na askari polisi wa Dawati la Jinsia. Siku hizo zitaisha kesho baada ya kuongezwa.
Akizungumza na vyombo vya habari juzi, Fatuma alisema yuko tayari kupima vinasaba na Lowassa ili kuthibitisha kama kweli ni baba yake na kwamba alimtafuta kwa muda mrefu bila mafanikio.
“Nilipeleka barua Ikulu kuomba kuonana na baba (Lowassa) kipindi akiwa Waziri Mkuu (2006-2008) lakini niliitwa mimi na mama katika klabu ya Mamba iliyopo Kinondoni,” alisema Fatuma.
“(Hapo) alikuja mwanaume akiwa kwenye gari lenye vioo vyeusi akatuhoji mimi na mama, akaondoka hakutupa majibu yoyote hadi leo.”
Kuhusu madai hayo, Lowassa alisisitiza kuwa kama kweli angekuwa mtoto wake asingesita kumchukua.
“Wala simjui, anasema ameshindwa kuniona wakati ana miaka 31, wewe unaamini kweli ameshindwa kuniona? Mbona wewe umenitafuta na umenipata na unaongea na mimi kwenye simu,” alisema Lowassa.
“Hizo ni siasa zinazolenga kuchafuana.”
Pia katika maelezo yake, Fatuma alidai kuwa aliwahi kukutana na mtoto wa Lowassa aitwaye Fred na alimwahidi kumsaidia lakini hadi sasa amekuwa kimya.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu