Lukuvi atangaza kiama.

In Kitaifa
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi, ametangaza kiama kwa wamiliki ardhi ambao hawajalipa kodi ya pango la ardhi na kutoa muda hadi April 30 mwaka huu kuhakikisha wanalipa kodi hiyo.
Waziri Lukuvi ameyasema hayo kwenye ziara mkoani Mwanza alipotembelea Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela na Halmashauri ya jiji la Mwanza na kuziagiza Halmashauri zote nchini kuhakikisha zoezi hilo la ukusanyaji wa kodi ya pango la ardhi linakamilika kwa wakati.
Amewataka wakuu wa idara za ardhi nchini kusajili hati za viwanja kwa wanaohitaji ardhi kwa kutumia majina yanayotambulika kwenye vitambulisho vya taifa NIDA ili kuepuka udanganyifu ambapo kodi hiyo ipo kisheria.
Waziri Lukuvi pia amezitaka Halmashauri zote nchini kuhakikisha wanapima maeneo yote yakiwemo mamlaka za viwanja vya ndege, hifadhi za wanyama na misitu taasisi zinazomiliki ardhi na wizara zote kupimwa.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu