Maafisa wakuu wa Shirika la Huduma ya Vijana kwa Taifa nchini Kenya amekamatwa kwa Ufisadi.

In Kimataifa

Mkuu wa Shirika la Vijana wa Huduma kwa Taifa nchini Kenya (NYS) Richard Ndubai, pamoja na maafisa wengine wakuu, wamekamatwa na polisi kwa tuhuma za ufisadi.

Hii inafuatia agizo la Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Umma aliyeagiza kushtakiwa kwa washukiwa wote waliotajwa katika kashfa ya Shilingi bilioni 9.

Maagizo ya Mkurugenzi wa mashtaka ya Umma Noordin Haji yametolewa baada ya kupokea taarifa kuhusu kampuni 10 na pia zaidi ya watu 40 binafsi waliotajwa katika sakata hiyo NYS scandal kutoka kwa Mkurugenzi wa uchunguzi wa Uhalifu George Kinoti.

“Mkurugenzi mkuu wa Mashtaka ya Umma amechunguza nyaraka zinazohusiana na sakata inayoendelea katika NYS na ameagiza mashtaka yafunguliwe mara moja dhidi ya wite waliotajwa kushukiwa ,” iliandika ofisi ya mwendesha mashtaka wa umma kwenye ukurasa wake wa Twitter Jumatatu asubuhi.

Washukiwa wengine kadhaa pia wamekamatwa na wanatarajiwa kufikishwa mahakamani katika kipindi cha saa 24, kulingana na afisa mmoja katika ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu