Maandalizi ya sensa ya majaribio 2021 yakamilika.

In Kitaifa

Ofisi ya Taifa ya Takwimu NBS imesema kuwa imekamilisha
maandalizi kwa ajili ya sensa ya majaribio ya mwaka 2021
inayotarajia kufanyika usiku wa kuamkia September 11 mwaka
huu.


Akizungumza kuelekea zoezi hilo Kamisaa wa Sensa kutoka
Zanzibar Balozi Mohamed Haji Hamza, amesema lengo la sensa
ya majaribio ni kupima mafanikio ya Sensa ya Watu na Makazi
ya mwaka 2022, na kuangalia changamoto ili kuzifanyia kazi
katika kipindi cha mwaka mmoja uliosalia kabla ya sensa
yenyewe.


Amesema sensa ya majaribio itafanyika katika mikoa 18
iliyochaguliwa ikiwemo mikoa 13 ya Tanzania Bara na mikoa 5
ya Zanzibar, na kutoa wito kwa mikoa itakayohusika katika
zoezi hilo kutoa ushirikiano wa kutosha ili kuhakikisha lengo la
Taifa linafanikiwa.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Tetesi za Soka Ulaya leo Alhamisi Septemba 23, 2021

Mshambuliaji wa Arsenal na Ufaransa Alexandre Lacazette, 30, hana hamu ya kusaini kandarasi mpya klabuni hapo. Mkataba wake wa

Read More...

Wanaharakati wa haki za binadamu wahoji hukumu dhidi ya Rusesabagina

 Makundi ya kutetea haki za binadamu barani Afrika yamelalamikia uamuzi wa mahakama kuu ya Rwanda ya kumfunga jela kwa miaka 25, Paul Rusesabagina ambaye alisifika sana kwenye filamu ya Hollywood ya Hotel Rwanda.  Mahakama hiyo Jumatatu ilisema kwamba imepata Rusesabagina pamoja na washukiwa wengine 20 na hatia ya

Read More...

LISSU NA WENZAKE WAFUTIWA KESI

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeifutia kesi ya uchochezi iliyokuwa inamkabili Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleao

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu