Maaskofu Anglikana waunga mkono jitihada za Serikali kukabiliana na Corona

In Kitaifa

Maaskofu wa kanisa la Anglikana  kutoka dayosisi 28 Tanzania bara na visiwani wamekutana jijini Arusha na kutoa tamko la kuunga mkono jitihada zote za serikali katika kukabiliana na ugonjwa wa Corona.
Akitoa tamko hilo leo jijini Arusha Askofu Mkuu wa kanisa Anglikana Tanzania,ambaye pia ni Askofu wa dayosisi ya Tanga,Askofu Dokta Maimbo Mndolwa alisema kuwa,kama kanisa wamejipanga kuendelea   kuunga mkono jitihada zote za serikali katika kukabiliana na ugonjwa huo kwa kushirikiana na wananchi na waumini wa kanisa hilo.
Askofu Mndolwa alisema kuwa,kanisa hilo katika kupambana na ugonjwa huo wanaendelea kufanya maombi ya mara kwa mara katika dayosisi  zote ,jumuiya na familia kwa ajili ya kumwomba Mungu kutuepusha na ugonjwa huo usiendelee kusambaa zaidi hapa nchini.


Alisema kuwa,wanaishauri serikali kuhimiza vyombo vya usafiri kuchukua hatua za tahadhari ikiwemo  kusafisha mabasi,ndege na maeneo ya usafiri .
“Tunaomba serikali kusimamia  mfumuko wa bei katika bidhaa muhimu na vyakula katika kipindi hiki cha mlipuko wa ugonjwa huo wa Korona.””alisema Askofu.
Askofu Mndolwa alisema kuwa,wao kama.kanisa wana imani kubwa kuwa hakuna lisilowezekana kwa Mungu ,hivyo wanaendelea kupiga magoti kutafuta uso wa Mungu katika kipindi hiki Cha kwaresma  ili asikie Sala zetu na kuturehemu.
Alisema kuwa ,kanisa linaelekeza kuwa kila dayosisi itenge siku maalumu ya maombi  kuanzia machi 19 kwa ajili ya kuombea ugonjwa huo ili Mungu aweze kuingilia Kati.


Askofu aliongeza kuwa ,kama kanisa kwa pamoja siku ya ijumaa kuu itakuwa siku ya ibada ya pamoja kanisa la Anglikana Tanzania kwa ajili ya kuombea  Taifa letu dhidi ya ugonjwa wa virusi vya  Corona 

“Tutaendelea kuwaombea wafanyakazi wote wanaotoa huduma kwa ajili ya  kuwahudumia wagonjwa wa Corona ili Mungu awaepushe na magonjwa hayo sambamba na kuwapa uvumilivu katika kuwahudumia .”alisema Askofu 

Aidha ugonjwa huo ulianzia nchini  China  desemba 2019 na kuenea sehemu mbalimbali hapa duniani,ambapo mpaka sasa hivi kwa Tanzania kuna wagonjwa watatu  wenye maambukizi ya virusi vya Corona

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WAGONJWA WA CORONA WAFIKIA 13 TANZANIA

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema idadi ya wagonjwa wa corona imefikia 13 ambapo kati yao 8 ni

Read More...

CORONA HAITAZUIA KUFANJIKA KWA UCHAGUZI – JPM

Rais Dkt. John Pombe Magufuli, amesema Ugonjwa wa Corona hautaizuia Tanzania kufanya Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu. Rais

Read More...

Mshtakiwa wa mauaji ya mfanyakazi wake wa Ndani, apandishwa kizimbani

Mshtakiwa wa mauaji ya mfanyakazi wake wa Ndani Mkami Shirima(30)Mkazi wa Sakina Arusha amefikishwa tena katika mahakama ya hakimu

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu