Magereza watoa ufafanuzi kuhusu Sugu.

In Kitaifa

Jeshi la Magereza nchini limetoa ufafanuzi kuhusu uamuzi wa mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph ‘Sugu’ Mbilinyi kuendelea kuvaa nembo ya namba yake ya mfungwa akiwa uraiani.

Jana, Sugu alihudhuria kikao cha 33 cha mkutano wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa amevalia nembo yenye namba yake ya mfungwa ambayo ni 219/2018, hali iliyowafanya wabunge wengi kumfuata, kuiangalia na kuteta naye.

Akizungumzia uamuzi huo, Afisa Habari wa Jeshi la Magereza, Lucas Mboje amesema kuwa jeshi hilo halihusiki na uamuzi wa Sugu kwani wao wameshamalizana naye, hivyo kuendelea kutumia nembo hiyo kunatokana na utashi wake.

Sugu ambaye alihukumiwa kifungo cha miezi mitano jela baada ya kukutwa na hatia ya kutumia lugha ya kufedhehesha dhidi ya Rais John Magufuli, aliachiwa kwa msamaha wa Rais alioutoa Aprili 26 kwenye sherehe za maadhimisho ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Akizungumza kwa mara ya kwanza Bungeni tangu Novemba mwaka jana, Sugu aliuliza swali la nyongeza akihoji kuhusu Sheria ya Huduma ya Habari ambayo alidai inakwenda kinyume na Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu uhuru wa vyombo vya habari.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

MBUNGE JAGUAR WA KENYA ALIYETISHIA KUWAFURUSHA WATANZANIA AKAMATWA

Maafisa wa polisi nchini Kenya wamemkamata mbunge wa jimbo la Starehe anayedaiwa kutoa kauli za chuki dhidi ya wafanyabiashara

Read More...

MANCHESTER CITY, YAMTOA KAFARA DANILO

. . Klabu ya Manchester City, ipo tayari kutoa kiasi cha paundi milioni 44 na beki wao wa pembeni

Read More...

TOTTENHAM MBIONI KUMSAJILI KIUNGO KUTOKA LYON.

. . Klabu ya Tottenham, imekubali kutoa kitita cha kiasi cha paundi milioni 62 kumsajili kiungo wa kati wa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu