Magufuli awatangazia neema Mabilionea.

In Kitaifa

Rais John Magufuli amesema, ana orodha ya kampuni hewa 17, 447 zilizojisajili Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) zinazofanya biashara hewa na kudai
kurudishiwa Kodi ya ongezeko la Thamani (VAT).

Rais Magufuli amesema anatamani atakapomaliza muda wake aache zaidi ya mabilionea 100 nchini.
Ameyasema hayo Ikulu jijini Dar es Salaam kwenye mkutano na wafanyabiashara kutoka wilaya zote nchini.
“Natamani inapofika mwisho wa kipindi changu cha uongozi, niache angalau mabilionea 100 nchini,” amesema.
Rais amesema, amekutana na wafanyabiashara nchini ili wajadili namna bora ya kuboresha mazingira ya biashara nchini.

“Serikali imeshaanza kuchukua hatua za kushughulikia baadhi ya changamoto zinazokabili sekta hii ya biashara na tumeshaandaa kitabu cha muongozo,” aliongeza

Kutokana na hilo ametoa siku 30 kwa kampuni hizo kulipa fedha wanazodaiwa serikalini.
Ameyasema hayo leo kwenye mkutano na wafanyabiashara unaofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Magufuli amesema lengo la mkutano huu ni kuzungumzia changamoto, mafanikio na maboresho ya kufanyika ili kuboresha mazingira ya biashara nchini.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

SOKA LA KIMATAIFA NA FUNUNU ZAKE

Real Madrid bado wanataka kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Brazili Neymar, lakini wanataka hakikisho kutoka Paris St-Germain kuhusu hali

Read More...

(TAMISEMI) KUTOA TANGAZO LA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA.

Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani S Jafo kesho tarehe 23 Mwezi

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu