MAGUFULI:Walarushwa wafungwe

In Kitaifa

Rais Dkt. John Magufuli, amesema anataka wala rushwa wengi wafungwe licha ya kuwa, kuna baadhi ya watu hawataki kusikia kauli hiyo.

Hayo yamesema  Ikulu Dar es Salaam baada ya kumwapisha Naibu Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Brigedia Jenerali John Mbungo.

Amesema wakifungwa wala rushwa nchi haitakuwa na rushwa kwani  ndio wamekuwa walimu wa walarushwa nchini,huku akiwataka viongozi hao wa Takukuru kwenda kusimamia kazi hiyo na wasimwogope mtu yeyote.

Rais Magufuli ameeleza kutoridhishwa na taratibu za uchunguzi na uendeshaji wa mashtaka ya rushwa yanavyochukua muda mrefu, na ametoa wito kwa viongozi wa Takukuru kufanyia kazi eneo hilo ili vita dhidi ya rushwa ionekane ikizaa matunda haraka.

Aidha amewataka viongozi wote nchini kushirikiana katika jukumu la mapambano dhidi ya rushwa ili kuepusha madhara ya tatizo hilo katika uchumi na ustawi wa jamii.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu