Mahakama yaamuru ‘Nabii Tito’ akapimwe Mirembe.

In Kitaifa
Mahakama ya Wilaya ya Dodoma imemuamuru mkuu wa Gereza la Isanga kumpeleka katika taasisi ya magonjwa ya akili mshtakiwa Onesmo Machibya maarufu Nabii Tito, ili kujua iwapo ana akili timamu au la.
Hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama hiyo, James Karayemaha ametoa agizo hilo leo Jumatatu Februari 19,2018.
Amesema Magereza wanachelewesha haki ya mshtakiwa na kwamba, anashangaa ni kwa nini wanashindwa kutekeleza agizo la kumpeleka kufanyiwa uchunguzi.
“Naagiza amri ya Mahakama itekelezwe, apelekwe taasisi ya magonjwa ya akili Isanga (Mirembe) si kama alivyoleta vielelezo kutoka Muhimbili,” amesema Karayemaha.
Hakimu ameahirisha kesi hadi Machi 5,2018 itakapotajwa kwa ajili ya kupokea taarifa ya uchunguzi.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu