Mahakama yaamuru Trump arudishe dola milioni mbili alizochukua.

In Kimataifa

Jaji wa jimbo la New York ameamuru Rais Donald Trump azirudishe dola milioni mbili alizozichukua kwa matumizi yanayotajwa na mahakama kuwa ni kinyume cha sheria.

Fedha hizo ni kutoka mfuko wa misaada wa ‘Trump Foundation’, ambapo inadaiwa kwamba alizichukua na kuzitumia katika kampeni zake kwenye uchaguzi wa mwaka 2016 uliomuingiza madarakani.

Uamuzi huu ni sehemu ya mashitaka yaliyowasilishwa na ofisi ya mwanasheria mkuu wa Jimbo la New York dhidi ya mfuko wa misaada wa ‘Donald J Trump Foundation’ akiwemo rais mwenyewe na watoto wake watatu Donald Junior, Ivanka na Eric.

Mahakama pia imeelekeza watoto wa rais Trump wanaosimamia uendeshaji wa mfuko huo kupatiwa mafunzo ya uongozi na kujua namna ya kufanya maamuzi ya matumizi ya fedha kwa misingi inayokubalika kisheria.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Mourinho kusuka kikosi chake.

Kocha mpya wa Tottenham Jose Mourinho atajaribu kumsajili tena mshambuliaji wa zamani wa Spurs Gareth Bale, 30, kutoka Real

Read More...

UNO ya Harmonize yawekwa private, Wasimamizi wa kazi zake waeleza.

Akizungumzia suala la kuripoti YouTube wimbo wa UNO, Magix amesema kuwa alimpa wiki moja Harmonize kumuomba msamaha kwa kutumia

Read More...

Bastola yadondoka na kuuwa mahakamani

Tukio la kusahangaza linalo Treand kwa sasa ni kuhusu kifo cha Mwendesha Mashitaka wa Serikali Afrika Kusini Addelaid Ferreira

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu