Mahujaji 35 waaga dunia wakifanya ibada Makkah.

In Kimataifa

 

Katika Ibada ya Hijja inayofanyika kila mwaka na kutekelezwa na Waislamu nchini Saudi Arabia katika Msikiti Mkuu mji wa Makkah eneo takatifu, Mahujaji 35 wafariki dunia.

Taarifa hizo zimetolewa rasmi na Wizara ya Afya nchini Misri, ambapo imesema kuwa siku ya kwanza ya ibada hiyo imepoteza Mahujjaji 35 kutokana na sababu ya uchovu na umri mkubwa.

Afisa mmoja wa Wizara hiyo, Ahmed el Ansary, amesema umri wa Mahujaji waliofariki ni kati ya miaka 60 hadi 85.

Katika Ibada hiyo ya Hijja mwaka huu zaidi ya Mahujaji milioni mbili wamehudhuria wakiwemo milioni 1.8 kutoka nje ya nchi.

 

Mahujaji hao wamekuwa wakifanya utaratibu huo wakifuata nyayo za Mtume wao Muhammad, aliyefanya utaratibu huo wa ibada miaka 1400 iliyopita.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu