Maiti za Virusi vya Corona China kuchomwa moto

In Kimataifa

Idadi ya vifo kutokana na janga la virusi vya corona nchini China imefikia watu 304
kufikia jana usiku, baada ya watu 45 wengine kufariki dunia, Serikali ya nchi hiyo imetoa
tangazo juu ya utaratibu mpya wa kuwazika waliofariki kwa kuwachoma moto.
Tume ya Afya nchini humo imesema vifo hivi vipya vilitokea katika mkoa wa Hubei,
ambao ndio kitovu cha mlipuko wa virusi hivyo. Kote nchini China, kulikuwa na
maambukizi mapya ya watu 2,590 jana Jumamosi na kufikisha 14,380 jumla ya idadi ya
watu walioambukizwa mpaka sasa.


Janga hilo limesababisha mataifa mengi kuwahamisha raia wao huku mashirika ya
ndege yakisitisha safari kwenda nchini humo.

Hatua hiyo pia inatishia kuathiri kwa kiasi kikubwa kushuka uchumi wa taifa hilo la pili
kwa ukubwa kiuchumi duniani. Kumeripotiwa zaidi ya visa 130 vya maambukizi ya virusi
vya corona katika karibu nchi nyingine 24 duniani

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

TUME YA MADINI KWENYE MKUTANO WA KIMATAIFA WA MADINI

Kamishna wa Tume ya Madini, Profesa Abdulkarim Mruma akielezea fursa zilizopo kwenye Sekta ya Madini Tanzania katika

Read More...

Halmashauri ya Jiji la Arusha kutokomeza mimba za utotoni.

Halmashauri ya Jiji la Arusha ikishirikiana na wataalamu wa Afya kutoka mashirika mbalimbali, maafisa  elimu kata na sekondari,

Read More...

MNADA WA ALMASI WDL WAZIDI KUPAMBA MOTO.

Leo tarehe 20 Februari, 2020 mnada wa asilimia tano ya madini ya almasi kutoka katika Mgodi wa Williamson Diamond

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu