Majaliwa aagiza mawaziri wakutane kuondoa mkanganyiko kwenye vyombo vya udhibiti hapa nchini.

In Kitaifa

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera na Uratibu, Bibi Jenista Mhagama akutane na mawaziri wa sekta nyingine na watafute namna ya kuondoa mkanganyiko uliopo kwenye vyombo vya udhibiti hapa nchini.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo Bungeni jijini Dodoma, kwenye mkutano wa 15 wakati akihitimisha hoja ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, taasisi zake na Mfuko wa Bunge kwa mwaka 2019/2020.

Amekuwa akitoa ufafanuzi juu ya masuala yaliyogusa vyombo vya udhibiti kama vile Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA, Shirika la Viwango Tanzania TBS, Mkemia Mkuu wa Serikali, Mamlaka nyingine za udhibiti pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA, OSHA, BRELLA na Taasisi ya Mionzi ambayo yaligusiwa na Waheshimiwa Wabunge.

Amesema licha ya Serikali kujenga mazingira wezeshi na rahisi ya kufanya biashara na uwekezaji, bado kumekuwepo na malalamiko kutoka kwa wafanyabiashara na wawekezaji kama walivyoeleza Waheshimiwa Wabunge wakati wa kuchangia hoja hiyo.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

MBUNGE JAGUAR WA KENYA ALIYETISHIA KUWAFURUSHA WATANZANIA AKAMATWA

Maafisa wa polisi nchini Kenya wamemkamata mbunge wa jimbo la Starehe anayedaiwa kutoa kauli za chuki dhidi ya wafanyabiashara

Read More...

MANCHESTER CITY, YAMTOA KAFARA DANILO

. . Klabu ya Manchester City, ipo tayari kutoa kiasi cha paundi milioni 44 na beki wao wa pembeni

Read More...

TOTTENHAM MBIONI KUMSAJILI KIUNGO KUTOKA LYON.

. . Klabu ya Tottenham, imekubali kutoa kitita cha kiasi cha paundi milioni 62 kumsajili kiungo wa kati wa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu