Majambazi waliomaliza vifungo na kuachiwa wapewa siku 7 kujisalimisha kwa mkuu wa upelelezi kanda Maalum.

In Kitaifa
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limetoa siku saba kwa majambazi wote waliowahi kutumikia vifungo na kuachiwa kwa kumaliza vifungo au rufaa, wajisalimishe kwa Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalumu.
Kauli hiyo ilitolewa jijini D ar  es  Salaam  na Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu, Lucas Mkondya wakati akizungumza na waandishi wa habari  ambapo  amesema lengo la kuwaita majambazi hao ni kutaka kupanga utaratibu mzuri ili waone kama baada ya vifungo vyao, wamebadilika na wanajihusisha na shughuli gani kwa sababu walikuwa ni majambazi sugu na walifanya matukio.
Aidha, Mkondya amewataka wenyeviti wa serikali za mitaa, kutoa taarifa kama kuna majambazi katika maeneo yao ambao wamechiwa, ili polisi wawafuatilie kikamilifu.
Hata hivyo Katika tukio jingine, jeshi hilo limewakamata watuhumiwa 44 wa wizi wa vifaa vya magari pamoja na vifaa hivyo vya magari ambapo  watuhumiwa hao walikamatwa kutokana na operesheni maalumu, ambayo inalenga kuwakamata wezi wa vifaa mbalimbali vya magari, ikiwa ni pamoja na wanunuzi wa vifaa hivyo katika sehemu mbalimbali za jiji hilo.
Operesheni hiyo iliyoanza Julai 18, mwaka huu na katika operesheni hiyo ambayo endelevu, watuhumiwa hao walikamatwa na baada ya kupekuliwa katika maduka yao walikutwa na vifaa mbalimbali vya magari.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu