MAJANGILI SUGU WAKAMATWA ARUSHA.

In Kitaifa

Jeshi la polisi mkoani Arusha kushirikiana na kikosi kazi kinachojihusisha na TANAPA, mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro, kikosi dhidi ya ujangili, KDU kanda ya kaskazini, panoja kikosi kazi taifa kinachopambana na ujangili kanda ya ziwa katika operesheni inayoendelea huko Loliondo kilifanikiwa kukamata  bunduki mbili za kivita panoja na risasi 15

Akizungumza na vyombo vya habari kamanda wa jeshi la polisi mkoani Arusha Jonathan Shanna amesema bunduki zilizokanatwa ni AK47 yenye namba 174364 ikiwa na risasi 6 ndani ya magazine pamoja na G3 yenye no A36011858 ikiwaa na risasi 9 ndani ya magazine ambapo bunduki zote zilikamatwa karibu na mpaka wa Tanzania na Kenya eneo la Naani tarafa ya Loliondo
Amesema Bunduki hizo zilipatikana  baada ya majibizano ya risasi baina ya kikosi kazi hicho kabambe na majangili mara baada ya kuona mashambulizi yamezidi, majangili hao walitelekeza silaha hizo na kukimbilia nchi jirani ya Kenya
Katika tukio lingine tena Jeshi la polisi mkoani Arusha kwa kushirikiana na TANAPA, mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro, kikosi shidi ya ujangili, mnamo tar10.11.2019 muda wa saa 08: 00 mchana katika eneo la la Olengusa kijiji cha na kata ya Oloipiri bdani ya eneo la pori Tengefu Loliondo wilayani Ngorongoro wilaya Ngorongoro katika msako mkali walifanikuwa kuwakamata watu 2 wanaojihusisha na ujangili ambao ni Nyamhanga Mwanga Mwita 19 na Chacha Marwa Mtocho 20 ambao wote ni wakazi wa  Serengeti Mara  wakiwa wameua wanyama aina ya Twiga
Amesema watuhumiwa hao walikamatwa wakiwa wanaendelea kuanika nyama hizo porini kwa ajili ya kusafirisha baada ya kuwa wamezikata vipande vipande
Katika tukio lingine maeneo ya Mbuyuniwilaya ya Arumeru mkoani Arusha jeshi la polisi limefanikiwa kuwakamata watu 5 wakiwa na meno 2 ya tembo
Watuhumiwa hao ni pamoja na Thomasi Sanjiro29, Edward Segeu Mollel 30 Emanuel Meyani 40, Lembris Lengasan 45, wote wakazi wa Simanjiro mkoani Manyara, na Samwel Jacob 53 mkazi wa Kingori wilaya ya Arumeru
Kamanda amesema katika tukio lingine watuhumiwa 2 wamekamatwa wakiwa wanatumia jina la Gavvana wa Benki kuu kuwatapelu watu kwa njia ya mtandao
Kamanda amesema watuhumiwa hao ni pamoha na Juma Hussein 33 Mnyiramba, kazi yake ni kusajili Line za simu na mkazi wa Sakina Arusha, Anan Gabriel Mbisse32 Mmeru mkazi wa Sombetini na Maji ta Chai mkoa wa Arusha, kwa tuhma za kutumia jina la Gavana wa Bank kuu Prf  Florance Luoga
Jeshi la polisi baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Gavvana kuhusiana na watu kutumia jona lake katika mtandao wa Fecebook na kisha kuwatapeli watu mbalimbali lilianza kufanya upelelezi wa acount yake na kupata no ya simu 0785349763 ambayo ilisajiliwa kupitia account hiyo ya kutumia hati ya kusafiria ya Norrish Andrew James raia ya Australia
Raia huyo wa Australia alifika nchini akitokea nchini Kenya na kufanya usajili kwa no ya simu kwa wakala aitwaye Juma Hussein ambapo wakala huyo alisajili laini za simu  ambayo walitumia kufanya uwalifu
Hata hivyo kamanda ametoa wito kwa watu wote wanaojihusisha na uwalifu wa mtandao kwani hawatabaki salama na wamejipanga vizuri kwa kuwakamata.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Mwenyekiti Bavicha taifa aomba udhamini ubunge.

Mwenyekiti wa Vijana Taifa chama cha Chadema John Pambalu amejitokeza kutia nia na kuomba udhamini kwa wanachama wa chama hicho katika

Read More...

RC Makonda amkaribisha DC Gondwe

Mkuu wa Mkoa DSM wa Paul Makonda leo July 9 amezungumza na Mkuu wa Wilaya mpya wa Temeke Mh Godwin Gondwe pamoja

Read More...

Takukuru Dodoma watoa kauli kuhusu mbunge kibajaji.

Kufuatia kuwepo kwa taarifa za TAKUKURU mkoani Dodoma kumshikilia mbunge wa Jimbo la Mtera Ndugu Livinstone Lusinde Kibabaji, leo wamezungumzia swala hilo. Kwa uzuri Mtaa wa Mastory

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu