Makamba Afunguka Sakata la Membe na Katibu Mkuu CCM.

In Kitaifa, Siasa
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi na Baba Mzazi wa January Makamba, Mzee Yusuph Makamba ameingilia kati sakata la Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM, Dkt Bashiru Ally kumuita hadharani kada maarufu wa chama hicho, Bernard Membe na kulitetea suala hilo ni la kawaida.
Kwa mujibu wa Makamba, utaratibu wa kuitana hadharani kwa viongozi wa chama hicho ni wa muda mrefu tangu enzi za TANU, na kubainisha kuwa yeye alishafanyiwa hivyo kwa zaidi ya mara moja.
“Mimi niliwahi kuitwa na John Mhavile, wakati nilipokuwa Mkuu wa Wilaya ya Tanga, kwa sababu yalitokea maneno pale Tanga niliambiwa njoo, tena si kwa simu, pia niliwahi kuitwa na Mwakawago kwa hiyo,  haya mambo hayajaanza jana,” amesema Makamba.
“Kwa hiyo kuitwa na wakubwa ni jambo la kawaida msiwaonee kwa njia waliyoitumia, Katibu Mkuu yuko sahihi, Katibu Mkuu amemuita Memba na aliyeitwa kakubali utaratibu ndiyo huo,” ameongeza.
Hivi karibuni kumezuka mvutano wa maneno baina ya Katibu Mkuu wa CCM Dkt Bashiru Ally, juu ya namna alivyotumia mikutano ya hadhara kumuita Membe jambo ambalo kupitia akaunti ya twitter, Membe alihoji njia hiyo.
Awali Dkt Bashiru alimuita Memba kwa ajili ya kujibu tuhuma zinazomkabili ikiwemo kupanga njama za kumkwamisha Mwenyekiti wa chama hicho ambaye pia ni Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.
Mnyukano umeonekana kuendelea tena kupitia mitandao ya kijamii ambapo kumekuwa na kampeni mbalimbali zikimtaja Bernard Membe kuwa mgombea Urais katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu