Makamu wa Rais azungumzia sekta ya afya nchini.

In Afya, Kitaifa

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan Serikali imedhamiria kuboresha huduma za afya nchini hasa huduma za mama na mtoto pamoja na kuboresha maslahi ya watumishi wa sekta ya afya.

Mapema leo Makamu wa Rais alianza kwa kufungua Jengo la Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima lenye vyumba 43 vya kufanyia kazi.

Makamu wa Rais aliweka jiwe la msingi la ufunguzi wa jengo la upasuaji lililopewa jina lake Samia Suluhu Hassan katika hospitali ya wilaya ya Maswa.

Akizungumza na wafanyakazi wa hospitali hiyo Makamu wa Rais alisema “ Serikali imedhamiria kuboresha huduma za afya nchini hasa huduma za mama na mtoto pamoja na kuboresha maslahi ya watumishi wa sekta ya afya, jitahidini kufanya kazi kwa bidii kwani kujituma kwetu kwa pamoja ndio ujenzi wa nchi yetu.”

Makamu wa Rais pia alipata fursa ya kuwahutubia wananchi kwenye uwanja wa Nguzo Nane wilayani Maswa ambapo aliwahakikishia wakulima wa pamba dawa za Viua Dudu zitapatikana kwa wingi na mapema kuanzia sasa na kati ya mwisho wa mwezi huu au mwanzoni mwa mwezi ujao.

Wakati huo huo Makamu wa Rais alipokea hundi ya shilingi 178,448,00 kutoka kwa Balozi wa China kwa ajili ya ujenzi wa bweni la wasichana wa shule ya sekondari ya Nkoma iliyopo wilaya ya Itilima pamoja na Vyerehani 50 kwa ajili ya Halmashauri ya Mji Bariadi.

Balozi wa China alimueleza Makamu wa Rais “ Simiyu ni mkoa unaokuja kwa kasi kwa maendeleo na Mkuu wa Mkoa na Viongozi wenzake wameonekana na nia ya kuleta maendeleo hivyo hatuna budi kusaidiana nao na kusaidia nia njema ya Rais Magufuli ya kuinua elimu na kujenga Tanzania ya Viwanda.”

Ziara ya mkoa Simiyu imekuwa na mafanikio makubwa kwani Makamu wa Rais alifungua Kongamano Kubwa la Elimu ya Juu na Uchumi wa Viwanda lililoandaliwa na Chuo Kikuu Husia cha Tanzania kikishirikiana na Uongozi wa mkoa wa Simiyu.Kongamano hilo lenye kauli mbiu ya “Mustakabali wa Elimu ya Juu kuelekea Tanzania ya Viwanda”

Makamu wa Rais alisema “ Tukizungumzia Viwanda tunazungumzia uongezaji wa mnyororo wamthamani ya mazao yetu na hivyo kuongeza pato la wananchi ambalo ndilo lengo kuu la Serikali”.

Akitolea mfano mkoa wa Simiyu ambao pamba yake asilimia 30% huchakatwa nchini na asilimi 70% hupelekwa nje ya nchi hivyo aliwataka Wataalamu kujiuliza ni vipi wahitimu wetu wamejipanga katika suala la uzalishaji Viwandani?.
Makamu wa Rais aliwataka waosmi waliokusanyika kwenye kongamano hilo watumie elimu yao katika kuhakikisha Tanzania ya Viwanda inawanufaisha watanzania zaidi.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Wanavikundi 500 wa kuweka na kukopa kanda ya kaskazini wakutana.

Zaidi ya wanavikundi 500 wa kuweka na kukopa kanda ya kaskazini wamekutana leo jijini Arusha lengo likiwa ni kupata

Read More...

Kijiji cha Ilkeren Kisongo chakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa maji

Kijiji cha Ilkereni kata ya Kisongo jijini Arusha kinakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa maji jambo linalopelekea wanafunzi wa

Read More...

SERIKALI KUIPATIA BILIONI MBILI KCMC KWA AJILI YA JENGO LA MIONZI

Dodoma Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeahidi kuipatia kiasi cha shilingi bilioni mbili

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu