Makonda kusajili ndoa zote mkoani kwake, aomba ushauri SADC

In Kitaifa

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda amesema kuwa atakuja na mpango wa kuanzisha mfumo wa kuhifadhi kumbukumbu zote za ndoa zilizopo mkoani mwake ili kupunguza utapeli wanaofanyiwa wanawake kwa kudanganywa na wanaume kuwa wataolewa.

Makonda amesema hayo leo Jumatatu Agosti 12, 2019, Huku akieleza kuwa  kuwa mbali ya mipango hiyo, Atatumia mkutano wa SADC  unaondelea nchini Tanzania kupata uzoefu kutoka kwa nchi nyingine kufahamu namna gani wanakabiliana na utapeli wa aina hiyo.

Kituo hicho cha kuhifadhi kumbu kumbu (Kanzi Data) kitahusisha usajili wa ndoa zote ili wanaume waliooa waweze kutambulika na kuwanusuru ili wasitapeliwe na kuumizwa mioyo yao kwa mifadhahiko ya kutegemea ndoa hewa.

Kanzidata hii itawasaidia wanawake wasitapeliwe, mtu akitaka kukuoa utaenda mtandaoni na kuangalia taarifa zake, utabaini kama ameoa au la na vilevile itawasaidia hata wanawake ambao wameolewa ili kuzuia waume zao wasioe kwa siri,” amesema RC Makonda.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

SOKA LA KIMATAIFA NA FUNUNU ZAKE

Real Madrid bado wanataka kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Brazili Neymar, lakini wanataka hakikisho kutoka Paris St-Germain kuhusu hali

Read More...

(TAMISEMI) KUTOA TANGAZO LA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA.

Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani S Jafo kesho tarehe 23 Mwezi

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu