MALIGHAFI ZA VIWANDANI 66% ZINATEGEMEA KILIMO,MIFUGO NA UVUVI- WAZIRI HASUNGA

In Kitaifa

MALIGHAFI ZA VIWANDANI 66% ZINATEGEMEA KILIMO,MIFUGO NA UVUVI- WAZIRI HASUNGA

Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga (Mb) leo tarehe 16.12.2019 amefungua Mkutano Mkuu wa Chama cha Wagani Tanzania (TSAEE) jijini Dodoma ambapo amewataka kuwasaidia wakulima,wavuvi na wafugaji nchini kuzalisha kwa ubora na kuongeza tija.

Waziri Hasunga amesema ili kufikia uchumi wa kati ifikiapo mwaka 2025 ,wataalam wa ugani wana jukumu la kusimamia uzalishaji kwa kutoa elimu ya kanuni bora za uzalishaji mazao ya kilimo ,mifugo na uvuvi kwa wingi.

Amesema Maafisa ugani wana jukumu kubwa kusaidia sekta za kilimo,mifugo na uvuvi kuongeza malighafi katika viwanda nchini.

“Asilimia 66 ya malighafi zote za viwandani zinatokana na kilimo,mifugo na uvuvi nchini Tanzania” alisema Waziri Hasunga.

Ili kufikia mafanikio hayo nchi ina changamoto ya uhaba wa maafisa ugani ili wafikie wakulima na wafugaji vijijini.

” Takwimu zinaonyesha maafisa ugani kilimo wapo 7,304,mifugo 3,795 na uvuvi 419 wakati nchi ina vijiji 12,319 kata 3,957 na mitaa 4,263″ alisema Waziri huyo

Hasunga amewahakikishia maafisa ugani hao kuwa kauli aliyoitoa Rais Dkt.John Pombe Magufuli hivi karibuni jijini Mwanza kuwa kipaumbele namba moja cha serikali kitakuwa kilimo,mifugo na uvuvi.

Amesema kupitia kauli hiyo wizara ya kilimo inampongeza Rais Magufuli kwa kauli yake hii ,hivyo changamoto zilizopo sasa zitatuliwa na serikali mapema na maafisa ugani wafikie malengo ya usimamizi wa sekta ya kilimo.

Katika hatua nyingine Waziri Hasunga amewaagiza maafisa ugani kuhakikisha wanakuwa na daftari la kumbukumbu ya wakulima aliowahudumia kila siku .

Pili amewataka wajiendeleze kitaaluma ili waweze kutoa elimu na ushauri bora kwa wakulima,wafugaji na wavuvi kutumia teknolojia ya kisasa kuongeza tija na hatimaye kuongeza soko la wakulima .

Kwa upande wake Afisa Kilimo Halmashauri ya wilaya ya Karagwe Adam Salum ameiomba wizara ya kilimo kukutana na wizara za kisekta kama Tamisemi ili kutatua changamoto za maafisa ugani nchini.

“Kuna baadhi ya maafisa ugani wetu wanaongozwa na wakulima kwa kuwa wakulima wana ujuzi zaidi katika uzalishaji,hii aibu .” alisema Afisa kilimo huyo akisisitiza umuhimu wa mafunzo kwa maafisa ugani.

Chama cha Maafisa Ugani ( TSAEE) kinaundwa na maafisa ugani kilimo,mifugo na uvuvi toka wizara zote za kisekta .
Mwisho.

Imeandaliwa na ;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Kilimo,DODOMA

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu